Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Coastal
Union yenye maskani yake jijini Tanga, umesema umejipanga imara kuhakikisha
kuwa wanafanya vizuri katika patashika ya Ligi ya Tanzania Bara, itakayoanza
Agosti 24 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union, Bin Slum, akiwa ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Coastal inaendelea na mazoezi
makali ya kujiweka fiti kwa ajili ya kuifanya timu yao ilete ushindani katika
msimu huu, sambamba na kuliwania taji hilo linaloshikiliwa na Yanga.
Akizungumza jana kwa njia ya
simu, Mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Aurora, alisema kuwa vijana wao
wanafanya mazoezi makali, pamoja na kucheza mechi nyingi za kirafiki.
“Tunaingia uwanjani kucheza
mechi za kirafiki mara kwa mara, tukiamini kuwa ni sehemu ya maandalizi yetu kwa ajili ya ligi,”
alisema Aurora.
“Tunaamini kuwa mambo yetu
yatakuwa mazuri kwa ajili ya kulinyakua taji la Ligi, ambapo mipango ni
kuhakikisha kuwa sisi tunafanya vyema, hivyo tunaamini suala hili litafanikiwa
kutokana na mipango,” alisema.
Ili kuboresha kikosi chao,
Coastal iliwaongeza wachezaji kadhaa akiwamo Haruna Moshi Boban na Juma Nyoso,
moja ya wachezaji wenye uwezo na majina ya kutosha katika ligi ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment