Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BENDI ya FM Academia,
maarufu kama Wazee wa Ngwasuma, imesema kuwa imeamua kuelimika na kuziba midomo
ya majigambo, kwasababu si njia za kuwaweka kileleni.
Ngwasuma inayoongozwa
na Rais wa Vijana, Nyosh El Sadaat, imeyasema hayo jana kwa kupitia Mkurugenzi
wake wa Fedha na Utawala, Kelvin Mkinga, ikisema kuwa majigambo hayawezi
kuwaletea heshima katika muziki wa dansi.
Mkinga alisema kwa
miaka kadhaa sasa, bendi ya FM Academia imezidi kufanya vizuri bila kuzalisha
malumbano ya mara kwa mara na wanamuziki wao, pamoja na kufunga mdomo wao.
Alisema kuna bendi
zinazojiendesha kwa majigambo, lakini jukwaani wanakuwa wepesi, hivyo kuwa njia
za kuwadhalilisha na kuwavunjia heshima mbele ya jamii.
“Tunashukuru
kwasababu sisi tunataka kazi na sio majigambo ya mara kwa mara hasa katika
vichwa vya habari, ukizingatia kuwa mpango huo hauna mbolea katika tasnia ya
muziki wa dansi.
“Tunatunga nyimbo
nzuri pamoja na kufanya shoo za aina yake ambazo ndio sababu ya kuiweka
kileleni bendi yetu, hivyo hatuwezi kuacha msingi wa kazi zetu,” alisema.
Wazee wa Ngwasuma kwa
sasa inatamba na wimbo wake wa Otilia, ulioimbwa kwa hisia za aina yake kutoka
kwa waimbaji wake, akiwamo Patchou Mwamba, Pablo Masai na wengineo.
No comments:
Post a Comment