Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema
mechi yao ya kirafiki ya Kimataifa dhidi ya Sport Club Villa ya nchini Uganda
ni muhimu kwa ajili ya kumpa kocha nafasi ya kuangalia mapungufu yao kabla ya
kuanza patashika ya Ligi ya Tanzania Bara itakayoanza Agosti 24 mwaka huu.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto, pichani.
Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na
mashabiki wa soka hapa nchini, imepangwa kuanza kutimua vumbi saa 10 za jioni
katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ambapo wadau wao watajionea
burudani ya aina yake.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kocha wao Ernest
Brandit, atapata fursa ya kuangalia uwezo wa vijana wake kabla ya michuano
kuanza.
Alisema kabla ya ligi hiyo kuanza,
Yanga pia itaingia uwanjani Agosti 17 kucheza mechi ya kuwania Ngao ya Hisani
dhidi ya timu ya Azam FC,iliyoweka kambi nchini Afrika Kusini.
“Ni mechi kali ya kirafiki dhidi ya
Sport Club ya Villa ya Uganda, huku kiingilio cha chini kabisa kwenye mchezo
huo kikiwa shilingi 5000 kwa mzunguuko ili kutoa fursa kwa mashabiki kuingia
kwa wingi zaidi.
“Tunaamini kocha wetu pamoja na
benchi lote la ufundi litapata fursa ya kushuhudia makali na mapungufu ya
wachezaji wao ili waone namna ya kuboresha kwa ajili ya kuleta ushindi katika
mechi zijazo,” alisema.
Yanga tayari imejigamba kujiandaa
kikamilifu kwa ajili ya kutetea taji lao ililotwaa msimu uliopita kutoka kwa
mtani wao wa jadi, Simba SC, huku nafasi ya pili ikienda kwa Azam
watakayokutana nayo kugombea ngao ya Hisani.
No comments:
Post a Comment