Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
SHIRIKISHO la Soka
nchini (TFF), limeshangazwa na uongozi wa Yanga kuitisha mkutano wa dharula ili
watowe uamuzi wa kukubali udhamini wa Azam tv au wakatae.
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura, pichani
Akizungumza jana
jijini Dar es Salaam, Msemaji wa TFF, Boniface Wambura, alisema Yanga inapoteza
muda na kujitwisha mzigo wa bure katika kufikiria la kuonyeshwa mechi zao Azam
TV.
Alisema viongozi wa
Yanga walikutana na Kamati ya Ligi na TFF kwa ujumla katika mkutano, hivyo
haina haja ya kulifikisha suala hilo kwa wanachama wao.
“Inashangaza mno,
maana mambo mengine yanafaa kuamuliwa na uongozi tu, hivyo sijui kwanini hawa
Yanga wanajitwisha mzigo mzito wa bure tu kwa huo mkutano wao wa Agosti 18,
katika Ukumbi wa PTA Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
“Sasa kuna haja gani
kila suala linalohitaji viongozi kuacha kuamua jambo kwa ajili ya kulipeleka
kwa wanachama wao bila sababu za msingi, ukizingatia kuwa wao ndio viongozi wa
Yanga,” alisema.
Suala la Azam tv
limeleta mkanganyiko kutoka kwa klabu ya Yanga, baada ya kugomea mechi zao
kuonyeshwa kwenye Kampuni ya Azam TV, wakisema sheria hazijafuatwa wakati wa
kutoa tenda hiyo kwa kampuni inayomiliki timu ambayo nayo inashiriki Ligi ya
Tanzania Bara.
Klabu 13
zinazoshiriki ligi hiyo zimeafiki kuonyeshwa mechi zao katika Azam TV,
isipokuwa Yanga inayoendelea kuweka msimamo wao juu ya ofa hiyo kutoka kwa
Kampuni hiyo nchini.
No comments:
Post a Comment