Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MBUNGE wa Ilala Mussa
Azzan Zungu leo amefungua semina kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza
Tanzania Bara kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kusema uchawi katika mpira hakuna.
Zungu alisema hayo
wakati akifungua semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam.
Alisema mpira unataka
maandalizi mpira wa miguu unahitaji maandalizi na pesa na kwamba pia unahitaji
ghrama kubwa ili kuuendesha.
“Miaka ya nyuma
tulikuwa tukicheza mpira kienyeji ingawa kulikuwepo na sheria 17, sasa msione
wale wanaoshindwa kucheza hawajui, tatizo hawajawekeza na ndio maana washuka
madaraja,” alisema.
Zungu pia alitumia
fursa hiyo kumpongeza nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwa
kutojisikia na kuhudhuria semina hiyo licha ya uchovu wa mechi ya jana ya Ngao
ya Hisani dhidi ya Azam walioshinda bao 1-0.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kassongo alisema bado ataendelea kupambana na
kutowaangusha wadau wa mpira wa miguu Mkoa wa Dar es Salaam.
“Nipo katika
mapamabano ya mpira kwa muda mrefu na nitahakikisha timu mojawapo ya Dar es
Salaam inaendelea kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom.
No comments:
Post a Comment