Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
TAMASHA
la burudani la kila mwaka linalojulikana kama Fiesta, limepangwa kuanza kutimua
vumbi Agosti 17 mwaka huu, huku likianzia mkoani Kigoma na wasanii mbalimbali
kutarajiwa kupanda jukwaani.
Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, pichani.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media
Group, Ruge Mutahaba, ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo, alisema tamasha
hilo litafanyika Kigoma kwa mara ya kwanza.
Alisema
lengo la kupeleka tamasha hilo mkoani Kigoma ni kupanua wigo wa kiburudani,
sambamba na kutafuta fursa kwa Watanzania wote, hasa mkoani Kigoma kwenye
changamoto lukuki.
“Kigoma
kuna fursa nyingi lakini zinashindwa kuonekana, hivyo hili ni jambo ambalo sisi
Clouds tumeamua kuanzia Fiesta huko kwa ajili ya kushirikiana na wadau kusaka
maendeleo ya wananchi wote.
“Ukiacha
Fiesta, lakini pia tutakuwa na ule mpango wa semina za ‘Twenzetu’, huku
tukiamini kuwa mambo yatakuwa mazuri kwa kuhakikisha kuwa watu wanafanya
harakati za kimaisha,” alisema.
Mara
baada ya kuzinduliwa rasmi mkoani humo, tamasha la Fiesta litaendelea katika
mikoa kdhaa ya Morogoro, Mwanza, Shinyanga, Tanga, Arusha, Iringa, Mbeya na
kwingineko.
No comments:
Post a Comment