UONGOZI
wa klabu ya Yanga, chini ya mwenyekiti wao Yusuf Manji, umeitisha Mkutano Mkuu
wa dharula uliopangwa kufanyika Agosti 18 mwaka huu, katika Ukumbi wa PTA
Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto.
Ajenda
kuu katika mkutano huo ni kutafakari kwa kina namna ya kuiweka Yanga yenye
ushindi sambamba na maazimio ya kuonyesha mechi katika Kampuni ya Azam TV, kampuni wanayosema ni ndogo haiwezi kupewa jukumu la kuonyesha mechi hizo.
Pia Yanga wanasema Azam imepewa haki hiyo bila kugombania tenda kama inavyojulikana, jambo ambalo linaweza kuibua mkanganyiko wa aina yake katika soka la Tanzania.
Mkutano
huo ni mwendelezo wa msuguano kutoka kwa Yanga wanaosita mechi zao kuonyeshwa
kwenye Azam tv, huku wenyewe wakisema kuwa wapo watu wanaoshinikiza suala hilo.
No comments:
Post a Comment