Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI
wa klabu ya Simba, umesema kuwa mpango wa udhamini wa kuonyesha mechi kwenye
Azam TV utakuwa na maanufaa makubwa katika soka la Tanzania, hasa kwa timu
zisizokuwa na uwezo kujikimu kiuchumi.
Hayo
yamesemwa na Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga, ikiwa ni siku chache baada ya
klabu ya Yanga kutangaza kutoutambua udhamini wa Azam katika kuonyesha mechi
zao.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Kamwaga alisema kuna timu zinazohitaji udhamini,
hivyo kuanza kuangalia namna ya kuufanya mpango wa Azam TV ufe, ni kuathiri
mfumo wa soka letu.
Alisema
wao Simba wamekubali kuingia kwenye udhamini huo kwasababu una malengo ya
kukuza soka letu, hasa kwa kuangalia fedha zinazopatikana zinaingia kwenye
mifuko ya timu husika.
“Kuna
timu zinashiriki ligi kwa ugumu kutokana na kukosa bajeti za kuwafanya
waendelee kusafiri na kuweka maandalizi ya mechi zao, hivyo naamini mpango huu
utakuwa na tija kwao.
“Huu ni
mpango mzuri kwa timu zote zinazoshiriki ligi hiyo, hivyo naamini tunaelekea
katika hatua sahihi hasa kwa timu zilizokuwa zinakabiriwa na matatizo ya kifedha,”
alisema.
Hata
hivyo, mpango huo unaendelea kupingwa na timu ya Yanga mechi zao kuonyeshwa
kwenye Azam tv, huku Shirikisho la soka nchini (TFF), likiwataka Yanga
waendelee na msimamo huo kwa mechi zao za nyumbani tu.
No comments:
Post a Comment