Mkugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt.
Charles Kimei, akizungumza na wadau mbalimbali katika akizindua Mikopo ya
nyumba ijulikanayo kwa jina la Jijenge itakayotolewa na benki hiyo, Dar es
Salaam jana.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WATEJA wa benki ya CRDB na
Watanzania kwa ujumla, sasa wanaweza kupata nyumba kwa urahisi, endapo wataamua
kujiunga na huduma mpya ya Jijenge iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam.
Katika huduma hiyo mpya, mteja
wa CRDB anaweza kukopa fedha za kujenga nyumba ya kisasa, kukarabati au kununua
na kutakiwa kulipa katika kipindi cha miaka 20.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk Charles
Kimei, alisema wameamua kuanzisha huduma hiyo ili kuwakomboa Watanzania katika
kipindi cha ukosefu wa nyumba bora za kuishi.
Alisema kuwa Watanzania wengi
wamekuwa na changamoto za kukosa makazi bora ya kuishi, hivyo yoyote anaweza
kuchukua mkopo wa kununua nyumba, kujenga au kukarabati na kutakiwa alipe
katika kipindi cha miaka 20.
“Hii ni hatua ya CRDB kuboresha
makazi ya Watanzania wote, ukizingatia kuwa kumiliki nyumba kwa Dunia ya leo ni
mtihani mkubwa kutokana na ugumu wa maisha.
“Kinachotakiwa ni kufika kwa
tawi lolote la CRDB na kuonyesha kiwango cha mshahara wako, huku mtu kuanzia
mwenye mshahara kuanzia 200,000 akiwa na sifa ya kupata mkopo,” alisema.
Aidha, Kimei alisema sio
waajiriwa tu, ila hata wajasiriamali nao wanaweza kupata mkopo huo ambao
umeanzishwa kwa ajili ya kuboresha makazi ya Watanzania wote.
No comments:
Post a Comment