Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BODI ya Miss Utalii Tanzania, imetangaza kusimamisha
kufanyika kwa mashindano hayo katika kipidi cha mwaka 2013/2014, lengo likiwa ni kujipanga upya na kuboresha mfumo
wa uendeshaji na
usimamizi wa ngazi zote.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo, alisema kuwa uamuzi huo ni mgumu kuchukuliwa na bodi ya mashindano hayo yenye kuheshimika katika viunga mbalimbali vya nchi hii.

Alisema kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya kikao cha
tathimini ya mashindano hayo tangu kuasisiwa kwake, huku akiamini kuwa kwa
kusimamisha kwa kipindi kifupi, wadau wote watakaa chini kuangalia changamoto
zinazowakabili.
“Fainali za kwanza za Miss Utalii Tanzania zilifanyika mwaka
2004 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam, ambapo
hapo historia ya Utalii ilianzishwa, hivyo tunaamini hizi ni changamoto
tunazoangalia kwa kina,” alisema Chipungahelo.
Kwa mujibu wa Chipungahelo, bodi katika tathimini hiyo ya
ndani imebaini changamoto mbalimbali za kimfumo, udhamini, utendaji, kuporomoka au kudumaa kwa sanaa ya urembo nchini, yakiwamo mashindano yao ya Miss Utalii Tanzania.
No comments:
Post a Comment