https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Saturday, January 18, 2014

Ipitie historia ya Wazigua kutoka wilayani Handeni mkoani Tanga

Picha mbalimbali zinaonyesha historia nzuri ya Tanga.
Hassan Abdallah na Andrew Kizenga Shundi
MBELWA, Chifu wa Wazigua mkoani Tanga, ndiye aliyekuwa mtawala wa jadi wa kwanza kutia saini mkataba na Dk. Karl Peters na kusababisha mkoa wa Tanga na eneo la bahari ya Hindi kutawalika na kuwa koloni la Kijerumani…………….ENDELEA..
TUWAKUMBUKE MASHUJAA WETU WA TANGA!
CHILO MWANA MACHAU na wenzake...katika miaka 1812..1830 kiliibuka mashujaa waliowapinga" WAJERUMANI ..WAKORONI"
shujaa wa Kizigua aliye Leta sifa kubwa na nikati ya mashujaa wa kizigua ambae aliupinga kwa nguvu zote ..utawara au uingiaji wa WAJERUMANI
"chiro mwanamachau " na wenzie walipo bainika kuwa wao ni kikwazo kwao waliwaua kwa kuwanyonga maeneo ya mjesani huko Tanga.
si hilo tuu Bali wajerumani walitoa tishio kwa wazigua endapo wataendelea kuwapinga utawala wao watawanyonga kama walivyo wanyonga wakina chilo mwana mchau na wenzake hii ni hadibhi fupi ya mashujaa wa kizigua.

Bwana Heri bin Juma alikuwa sultani wa Saadani iliyokuwa bandari ya biashara kwenye mwambao wa Bahari Hindi Tanga katika Tanzania kaskazini-mashariki tangu
miaka ya 1870.

Mtawala wa Saadani

Alitawala chini ya Sultani wa Zanzibar kama mkubwa wake lakini akafaulu kutetea nafasi yake kama sultani aliejitegemea. 1882 aliweza kushinda jeshi la Sultani Sayyid Bargash aliyetaka kutawala Saadani moja kwa moja. Saadani kama miji mingine ya pwani ilifaidika na biashara ya Wazungu walioleta bidhaa na kulipa ushuru. Alielewana vema nao.

Kuja kwa Wajerumani

1886 Sultani Sayyid Khalifa wa Zanzibar alikodi eneo lake katika Tanganyika bara kwa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki. Bwana Heri pamoja na viongozi wengine aliona amesalitiwa na Sultani hakuwa tayari kukubali utawala wa Wajerumani. 1888

Vita ya Abushiri

Bwana Heri aliunga mkono na upinzani wa Abushiri dhidi ya Wajerumani akipata usaidizi wa makabila wa eneo lake hasa WAZIGUA. Akiwemo shujaa maarufu wa kizigua aliyejulikana kwa jina la Senkondo Mwechiwa,

Alishambuliwa na kiongozi Mjerumani Hermann von Wissmann aliyekuwa na silaha za kisasa akapaswa kuacha kambi yake Saadani tar. 6 Juni 1889. Aliendela na vita ya msituni. Baada ya kushambuliwa tena na jeshi la Wajerumani katika Januari na Machi 1890 uwezo wake ulikwisha. Sayyid Khalifa aliwasiliana naye na Wissmann akatayarisha kujisalimisha kwake tar. 6 Aprili 1890. Wissmann aliyemheshimu Bwana Heri hakumwua kama Abushiri bali akamwambia kujenga Saadani upya.

Upinzani wa wenyeji na utawala wa KIZIGUA ulishindwa lakini ulisababisha mwisho wa utawala wa kampuni iliyoshindwa kukandamiza uasi wa Waafrika. Serikali ya Ujerumani iliona haja ya kungilia kati na kuchukua utawala wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani mkononi mwaka kama koloni ya serikali ya Ujerumani.
Mwisho wake

Mwaka 1894 alijaribu kwa kushirikiana na utawala wa kizigua tena kupambana na Wajerumani lakini alishindwa kwa mara ya pili. Akaondoka bara kwenda Zanzibar alipokufa baadaye.

KUINGIA KWA WAZIGUA SOMALIA
Asili ya Wazigua waishio Somalia: pamoja na asili fupi ya Wazigua,baada ya Mjerumani kuweza kutawala eneo la ukanda wa bahari ya Hindi na maeneo ya Tanga hali hii ilipelekea………………………………..INAENDELEA

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...