Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MAENEO ya Kimara, jijini Dar es
Salaam, kumetokea mkanganyiko baada ya misikiti kuwa na mtazamo tofauti juu ya
kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kuipokea Sikukuu ya Idd.
Mtazamo huo pia upo katika
maeneo mengi ndani na nje ya nchi, hususan kutokana na imani kuamualiwa na watu
wachache, hivyo kupoteza ladha na utetezi wa dini ya Kiislamu, hasa nyumba ile wanaswali na wale wanasubiri kesho kwa ajili ya kuusubiri mwezi hapo jioni ya leo.
Hata hivyo, idadi kubwa ya
Waislamu wanaswali Sikukuu ya Idd kesho Ijumaa badala ya leo kama wanavyofanya
baadhi yao.
“Sisi kwetu Idd itakuwa kesho
Ijumaa, hivyo tunaomba waumini wa dini ya Kiislamu kuendelea na mfungo mtukufu
wa Ramadhan badala ya kusikiliza maoni ya watu wachache,” alisema sheikhe mmoja
ambaye hata hivyo hakuweka jina lake hadharani.
Handeni Kwetu inawatakia
waislamu wote Sikukuu njema ya Idd hapo kesho na kuwapa imani nzuri wengine
wote duniani.
No comments:
Post a Comment