Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
NI wazi
hakuna Tamasha kubwa la muziki hapa nchini, isipokuwa hili la Fiesta 2013,
linalotarajiwa kuanza kuwaka moto leo mkoani Kigoma, katika Uwanja wa Lake
Tanganyika.
Shoo hiyo
inayofanyika kila mwaka, uzinduzi wake unaanzia mkoani Kigoma, ambapo shughuli
itaendelea katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.
Ruge Mutahaba
Wadau wa
muziki wa Tanzania wamekuwa na shauku ya tamasha hilo kunaatokana na kusheheni
wasanii wenye uwezo wa juu wa kuimba na wenye mashabiki lukuki.
Linah, pichani
Wasanii
kama vile Barnabas, Mwana FA, AY, Madee, TID, Linah, Recho na wengineo
wamepangwa kuwapo katika uzinduzi huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wake.
Katika
kila mkoa wa Tanzania Bara, shoo ya Fiesta ndio pekee yenye mguso na
inayosisimua kwa kiasi kikubwa, ndio maana mara kadhaa imekuwa ikifanyika
uwanjani.
Katika
mazungumzo na Handeni Kwetu Blog yaliyofanyika juzi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media
Group, Ruge Mutahaba, anasema kuwa tamasha la Fiesta limeshakamilika kwa
maandalizi yake.
Mutahaba
anasema kuwa mambo mengi yameboreshwa ukiwamo mpango wa wasanii kupanda
jukwaani au mikakati ya ufanyaji shoo wenye kuwapa burudani mashabiki wao.
“Shoo ya
Fiesta ndio pekee yenye mguso kwa nchi hii, hivyo sisi kama waandaaji
tunachofanya ni kuweka mkazo na mguso katika kuandaa ili wadau wetu waburudike.
“Hakuna
kinachofanyika kwa sasa zaidi ya kuangalia Fiesta itakuwaje kwa msimu huu mpya,
huku mikoa mbalimbali ikitarajiwa kupata shoo hii, hasa mikoa ya Kigoma na
Mtwara,” alisema Mutahaba.
Ruge
anasema kuwa mikoa ya Kigoma na Mtwara inafanyika shoo hiyo kwa mara ya kwanza,
huku wakiamini kuwa italeta burudani na kuwaweka pamoja wadau wote.
Wakati
Kigoma shoo hiyo ikipangwa kufanyika kesho, wenzao wa Mtwara watapata burudani
ya tamasha hilo Jumamosi ya Agosti 31 na kushuhudia burudani hiyo.
Anasema
kwamba baada ya tamasha hilo kuzinduliwa rasmi mkoani Kigoma, watafuata wakazi
na wananchi wa Tabora, ambapo Agosti 23 nao wataburudika kwa idadi kubwa ya
wasanii waliopangwa kuwapo katika tamasha hilo la aina yake.
Mikoa
mingine ambayo itapata shoo hiyo ya Fiesta ni pamoja na Singida, Mwanza,
Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga, Arusha, Moshi, Musoma na Shinyanga.
Katika
hatua nyingine, Mkurugenzi huyo wa Utafiti na Matukio wa Clouds, anasema kuwa
Fiesta pia imeongezwa mikakati ya kutafuta namna ya kuwapatia maisha bora
Watanzania.
Anasema
katika mkoa wa Kigoma, kabla ya shoo hiyo, pia watafanya semina na vijana kama
walivyofanya mkoani Dodoma katika uzinduzi wa ‘Twenzetu’.
Mkoa wa
Kigoma ambao una mambo mengi mazuri, lakini umekosa mwamko, ndio maana sisi kwa
pamoja tukaamua tuingie kwa ajili yaa kufuta tatizo hilo.
“Hii si
sahihi, hasa watu wanaposema kuwa mkoa wa Kigoma ni wa mwisho, wakati sisi
tunajua kuna mambo mengi yenye mwangaza kwa ajili ya maisha ya wakazi na
wananchi wao.
“Hii ni
sawa na Mtwara, hivyo tutakuwapo kwa mikoa hii miwili na mengine kwa ajili ya
kuhamasisha pia mbiu yetu ya Twenzetu iliyozinduliwa mkoani Dodoma mapema mwaka
huu,” alisema Mutahaba.
Anasema
juu ya masuala ya amani na utulivu ni jambo la kwanza sehemu zote wanazokuwapo,
jambo linalowafanya Watanzania waamini hakuna tamasha lingine lenye mguso na
mwanamko kama Fiesta.
Naye
Winfirda Josephat maarufu kama (Recho), alijigamba mno juu ya kuonyesha
manjonjo yake katika tamasha hilo la Fiesta litakalozinduliwa mkoani Kigoma.
Anasema
kuwa amejiandaa vizuri kufanya mambo makubwa katika tukio hilo linalokusanya
mashabiki wengi kwa wakati mmoja ili kufurahia muziki kwa ujumla.
Anasema
kuwa anaamini alichofanya katika tamasha la mwaka jana kitakuwa kidogo kati ya
vitu atakavyoonyesha katika burudani za Fiesta mwaka 2013.
“Sitaki
kuongea sana, maana najua sehemu ya kuonyesha mbwembwe ni jukwaani, hivyo
naomba wadau wote na mashabiki wangu waje kujionea vitu vya hali ya juu.
“Nipo
sawa na nimejiandaa kwa kipindi kirefu mno, huku nikiwa na kila sababu ya
kupanda jukwaani na kuwapatia shoo ya aina yake mashabiki wote wa tamasha
hili,” alisema.
Recho
anatamba na nyimbo kadhaa, ukiwamo wa Kizunguzungu, Upepo, Nashukuru Umerudi na
sasa ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Mwali Kigego.
Recho
anajulikana sana kwa kufuata nyayo za mkali mwingine wa muziki huo, Rehema
Chalamila, maarufu kama Ray C, ambaye mara kwa mara ameshindwa kuficha uhalisia
huo.
Mwanadada
huyo ametokea katika taasisi ya kukuza na kulea vipaji ya Tanzania House of
Talents (THT), kama ilivyokuwa kwa Linah, Barnabas, Mwasiti, Amini, Vida,
Mataluma na wengineo waliotokea kwa juhudi za taasisi hiyo ya muziki nchini.
No comments:
Post a Comment