Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NI Tanzania tu tunaoneana haya kuambiana ukweli, hasa hili
sakata la kuona wasanii wengi wa nyumbani, wakiwamo wa muziki wa kizazi kipya
wanavyotumbukia kwenye ubwiaji wa unga.
Msanii Diamond pichani.
Ni wavutaji wa dawa za kulevya. Tunaona jinsi
hali zao kiafya au mwonekano wao katika jamii. Katika nchi za wenzetu, hasa
nchini Marekani, kuambiana ukweli kwao ni jambo la lazima.
Ahmad Ally 'Madee'
Hapa kwetu mtu akiambiwa anakula unga, hata kama
ikiwa kweli, atakataa au wale wanaomzuungaka, yani marafiki zao kumtetea, hivyo
kumfanya aendelee na vitendo vyake.
Ney wa Mitego
Msanii Rehema Chalamila, maarufu kama Ray C yeye
alionekana shujaa mno alipoweka wazi. Hata hivyo si Ray C tu, ila wasanii wengi
wao wanabwia unga.
Marehemu Albert Mangweha Ngwair, aliripotiwa kuzidiwa na dawa za kulevya zilizosababisha kifo chake.
Kwa mfano, kusikia au kuona mtu akisema
hadharani Rihanna anakula unga au amefundishwa na swahiba wake Chris Brown ni
rahisi mno, wakiamini kuwa jamii itajifunza.
Msanii Dayna pichani anapaswa ajichnge na dawa za kulevya
Unga unatajwa kuwa ni ulevi wa ghali ila kuanza
kwake ni rahisi mno, huku kuacha kwake ikiwa kazi kubwa. Mtu anaweza kuanza
kuvuta unga kwasababu mbalimbali.
Chipukizi wa Bongo Fleva, Vida naye anastahili kujichunguza na matumizi ya dawa za kulevya
Sababu hizo kubwa ni mtandao wa marafiki
wanaotumia dawa za kulevya, hivyo mtu kuona kuna ulazima na yeye kuingia kwenye
ulevi huo ili wafanane kitabia na mtazamo.
Lady Jay De, licha ya kuwa nyota wa muziki, ila anaweza kuathiri kipaji chake endapo atajiingiza kwenye matumizi hayo.
Tunaweza kuchukulia kiurahisi, ila suala la
ulevi wa unga kwa wasanii wa Tanzania liahitaji nguvu za ziada na kuambiana
ukweli. Wengi wao ni waathirika wa hilo.
Msanii Rehema Chalamila, Ray C ni mwathirika wa dawa za kulevya na wengine lukuki ambao bado wanafanya siri.
Wasanii kama vile Langa Kileo ambaye kwa sasa ni
marehemu, alikuwa kwenye ulevi huo. Ingawa mwenyewe mwanzo alikataa, lakini
baadaye alikiri kula unga.
Profesa Jay mkali wa muziki wa Hip Hop Tanzania
Mwingine ni marehemu Albert Mangweha Ngwair
aliyefariki nchini Afrika Kusini, akihusishwa kuzidiwa na dawa za kulevya.
Ingawa ripoti yake ilivuja, lakini tulifanya kazi ya ziada kuuficha ukweli.
Mr Blue, alitamba sana wakati huo.
Hadi leo, hakuna aliyethubutu kuinua kinywa
chake kuweka wazi kifo cha Ngwair, tukiamini kuwa tunamdhalilisha marehemu. Hii
si kweli hata kidogo, maana woga wetu ndio chanzo cha kuhalalisha matumizi ya
dawa za kulevya kwa jamii.
Linah, msanii kutoka THT
Kila mtu anajua jinsi matumizi hayo
yanavyoharibu mfumo na mtazamo wa jamii, wakiwamo wasanii wanaotambulika kama
kioo cha jamii. Katika kuliangalia hilo, nathubutu kusema kuwa katika kila
wasanii 10, sita wanatumia dawa za kulevya.
Mara kwa mara tunaona jinsi baadhi yao
wanavyoshindwa kufanya shoo zenye kuvutia mashabiki wao. Muda wote yupo nyuma
ya jukwaa akivuta bange, unywaji wa pombe na kuchanganya na dawa.
Hilo ni jambo lenye kukera mno. Tuna hatari ya
kupoteza wasanii wetu kutokana na matumizi hayo mabaya. Hii inahitaji kupeana
elimu ya kutosha na kuambiana ukweli.
Tunaweza kumuona Ray C ni mtu wa ajabu mno,
lakini kuna kundi kubwa la vijana wenzake katika Bongo Fleva wanaokula unga.
Kesho tutaona aibu tutakapokosa nguvu kazi ya Taifa kwasababu ya kuathiriwa na
matumizi hayo ya dawa za kulevya.
Kila mtu mwenye ukaribu na msanii wa Tanzania,
lazima amwambie ukweli swahiba wake huyo, ndugu yake kuwa ulevi wa unga hauna
thamani katika mwili na vipaji vyao.
Waache kwa ajili ya kujenga jamii bora. Ingawa
ulevi huo unauzwa kwa bei ghari mno, lakini pia unasababisha mkanyanganyiko katika
utendaji wa kazi kwa jamii na wasanii kwa ujumla.
Mlevi wa unga siku zote hapendi kusumbuka.
Anapenda kukaa na kujidunga wakati wote. Hata kama ana akiba ya Milioni 50
katika akaunti yake, lakini kwakuwa ni anakula unga, hakika hizo zitakwisha kwa
siku chache mno.
Wasanii hao ndio wale wanaoshindwa kabisa
kufanya kazi zao kwa ufanisi, tena wengineo wakiwa wazito kabisa kupanda
jukwaani. Msanii anajua kabisa kuwa ana shoo, lakini anapanda saa 9 usiku huku
akiwa kwenye ulevi wa kupindukia.
Akipanda jukwaani hana anachoimba na kushuka.
Kesho wasanii wenzake, mashabiki wake wanamuona mtu wa kawaida. Thamani yake
inapotea na kuanza kuwashika uchawi wenzake.
Ndio maana nasema, wasanii wengi wanakula unga.
Kulisema hili hatuhitaji kupata kibali cha Polisi, ukizingatia kuwa watu hao
wanajulikana mwenendo wao kwa ujumla.
Tuwaambie ukweli, tuwakataze bila kuwaonea haya
kwa ajili ya kujenga jamii bora, maana kila siku ya Mungu hali inazidi kuwa
mbaya na kuwaweka wasanii mtegoni.
Dawa za kulevya ni tatizo kwa wasanii wetu.
+255 712 053949
No comments:
Post a Comment