https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, August 28, 2013

Mkuu wa shule ya sekondari ya Kwamatuku wilayani Handeni aelezea mikakati ya shule yao



Na Mwandishi Wetu, Handeni
MKUU wa shule ya Sekondari ya Kwamatuku, iliyopo Kata ya Kwamatuku, wilayani  Handeni, mkoani Tanga, Faustine Mroso, amesema pamoja na changamoto wanazokutana nazo, lakini shule yake imejipanga imara kuwapatia wanafunzi elimu bora.
Mroso ameyasema hayo siku chache baada ya kuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne, waliotia hofu ya ufindishwaji katika shule hiyo.

Akizungumza na Handeni Kwetu Blog, Mroso alisema kuwa si kweli kama shule yake haifundishi vizuri, hivyo wanafunzi hao waendelee kujiandaa kwa kusoma kwa bidii, huku uongozi wa shule yake ukiwa umejipanga imara kuwaandaa wanafunzi hao.

Alisema shule yake ilikaguliwa mapema mwaka huu na kuonekana ina mipango kabambe yenye maendeleo ya kielimu, hivyo kinachosemwa dhidi ya wanafunzi hao si kweli.

"Mimi  katika shule hii si mwenyeji, maana nimekuja mapema mwaka huu, hivyo naomba wanafunzi wanipe ushirikiano kwa lolote linalotokea kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanajiandaa vizuri kwa ajili ya kupata matokeo mazuri,” alisema Mroso.

Kwa mujibu wa Mroso, shule yake ina uongozi mzuri pamoja na mipango ya kuwaandaa vyema wanafunzi, ikiwa ni njia nzuri ya kuhakikisha kuwa wanakuwa katika nafasi nzuri.

Awali, baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo walilalamikia uongozi wa shule kwa madai kuwa ufindishwaji wao si mzuri na unaweza kuwaweka katika nafasi mbaya kwenye mitihani yao ya kidato cha nne baadaye mwaka huu.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...