https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, August 29, 2013

Mgombea udiwani mwaka 2010 kwa tiketi ya CUF sasa akichulia chama chake


Na Rahimu Kambi, Handeni
ALIYEKUWA mgombea udiwani Kata ya Kwamatuku, wilayani Handeni, mkoani Tanga, kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Mwamini Andrew, amesema haoni sababu ya kubaki katika chama kisichokuwa na dhamira ya kuwaongoza Watanzania.
Mwamini Andrew, Mgombea Udiwani mwaka 2010 Kata ya Kwamatuku, wilayani Handeni, mkoani Tanga kwa tiketi ya CUF, pichani.

Mwamini ameyasema hayo wakati hivi karibuni aliuhakikishia mtandao huu kuwa ameamua kuachana na CUF na kuamua kurudi kuhamia katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na Handeni Kwetu Blog, Andrew alisema kwamba Watanzania wanahitaji kuongozwa vyema na kupatiwa maendeleo, hasa wale wanaoishi vijijini.

Alisema vyama vya siasa mfano wa CUF haviwezi kuwa na jipya kiasi cha kuwakomboa Watanzania, hivyo kwake yeye kuondoka ni jambo lenye mashiko kwa kiasi kikubwa.

“Niligombea udiwani kwa tiketi ya CUF, lakini kwa sasa hamu sina kutokana na changamoto nyingi zinazokikumba chama hasa mipango na ushirikiano kati ya wanachama na viongozi kukosekana.

“Naamini mipango yangu ilienda vizuri, huku nikiamini kuwa lengo ni kufanikisha maendeleo kati ya wananchi na serikali, sanjari na viongozi wa vyama vyote vya siasa,” alisema Andrew.

Kauli ya kijana huyo inaweza kuwa mwiba mkal kutoka kwa vijana wanaoamini kuwa chama cha CUF kimepoteza mvuto ndio maana wengi wamekuwa wakikihama kwa kasi ya ajabu.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...