MIMI ni mfuatiliaji
mzuri wa matukio kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ndani na nje yaa nchi, huku
pia nikiwa shabiki mkubwa wa muziki hapa nchini.
Msanii Diamond, akiwa kwenye poziiii
Pamoja na
kuwa na uhodari huo, lakini nachukizwa sana na mwenendo wa mitandao ya simu za
mikononi kuunganisha watu nyimbo bila kupenda.
Hii ni
kwasababu kuna watu ambao wamekuwa wakiunganishwa kwenye huduma hiyo ya muito
wa simu katika mitandao bila kuomba, hivyo kumsumbua au kumtia gharama
isiyokuwa na sababu.
Mimi ni
miongoni mwa watu wanaokumbana na tatizo hilo. Mtandao wangu ambao siutaji kwa
jina umekuwa ukinikata pesa eti wakisema wamechukua gharama ya wimbo wangu
unaosikika katika simu yangu.
Kwa
bahati mbaya, wimbo unaosemwa mimi sijaomba. Hata pale ninapopiga simu katika
mtandao wangu kuwataka waondoe huduma yao, wanaendelea kunifanyia udanganyifu.
Hakika
siwezi kukubaliana hata kidogo, hivyo lazima hawa wadau wenye makampuni hayo
wafuate utaratibu maana kwa sasa hali hii haiwezi kukubaliwa hata mara moja.
Kuna
wakati mtu unaumia kuona unatozwa fedha ambazo usingependa kukatwa kwa sababu
ya huduma ambayo si kila mtu anaipenda, jambo linaloleta mkanganyiko.
Huu ni
wakati ambao hawa wenye makampuni ya simu waone imetosha, hasa kwa kuhakikisha
kuwa baadhi ya huduma zao, zikiwamo za mwito wa akupigae zinatolewa kwa
wanaopenda tu.
Mariam
Jumaa
Kinondoni,
Dar es Salaam
Na wewe pia unaweza kututumia kero yako na sisi tutaipachika ili isomwe na watu wengi zaidi. Tuma kwa email kambimbwana@yahoo.com au +255 712053949.
No comments:
Post a Comment