Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
NI siku nyingine mimi
na msomaji wangu tunapokutana katika safu hii inayokujia kila Jumamosi,
ambapo tunachangia mambo mbalimbali yanayohusu uhusiano na maisha.
Wapendanao pichani.
Nashukuru kwako wewe
unayeguswa na safu hii na kuniunga mkono kila Jumamosi, nikiamini kuwa
nitaendelea kuwapo hapa.
Ndugu msomaji wangu,
kuna watu ambao katika uhusiano wao, kila siku wamekuwa wakiishi kwa malalamiko
makubwa kiasi cha kuwaondolea hamu ya kubaki kwenye uhusiano wao.
Hawa ni wale
wanapofikia muda wa kurudi majumbani mwao, hamu yote imekata. Wapo mabinti
ambao wamekosa hamu kabisa ya kuingiliana kimwili na wapenzi wao, wakiwamo wale
waliofanikiwa kufunga ndoa.
Kwa wale ambao bado
ni wapenzi au wachumba, si tatizo, ila mbaya zaidi hali hii ipo pia kwa watu
ambao wamefunga ndoa.
Utakuta mtu yupo na
amani na furaha tele. Lakini anapofikiria kasumba ya kitandani, tumbo
linamnyongolota.
Ukilifikiria suala
hili, utadhani labda watu wa aina hiyo wanaumwa. Ila hapana, maana baadhi yao
ni wavivu ama pia kuona ni uchafu.
Watu wanatofautiana,
ndio maana linapoingia suala la aina hiyo, kitu kinachotwa ndoa hakiwezi kuwa
na amani na kuwaridhisha wenzetu.
Kwa mfano, mwanaume
aliyebahatika kuwa kwenye ndoa na mwanamke asiyependa kitendo cha haki ya ndoa,
basi anaweza pia kushikwa na tamaa ya kujihusisha pia na watu wa nje.
Na sio mwanaume tu,
ila hata mwanamke akiwa anaishi nwa mtu mvivu asiyejua namna gani ya kumridhisha
mwenzake hawezi kufurahia ndoa.
Atakuwa na malalamiko
tu. Ndio maana hata muda wa kurudi nyumbani unapofika, ataendelea kujizunguusha
ili usiku uingie.
Hana cha kumuwahisha
nyumbani, maana anajua hata akirudi nyumbani kwake usipoangalia anakuta kelele,
au kutokupewa kile anachopenda.
Hii ni mbaya mno,
hivyo kuna haja sasa ya kila mtu kujitafakari anavyoishi na mume au mke wake,
kwa wale waliobahatika kufunga ndoa.
Sio kwa wana ndoa tu,
hata wale waliokuwa kwenye upenzi wa kudumu na wenye muelekeo wa kuwa mwili
mmoja, endapo uhusiano huo unahusisha tendo la ndoa basi ni wajibu kujiangalia
vuzuri.
Nasema hivi huku
nikijua kuwa Dunia ya leo, asilimia kubwa wanaofunga ndoa, basi lazima walikuwa
kwenye uhusiano.
Si kama zamani mtu
kufunga ndoa na msichana aliyemuona kwenye picha au aliyetafutiwa na ndugu zake
kijijini nay eye kuletewa mke tu.
Leo vijana wanapenda
kuonana kwanza ndio mambo mengine yafuate, ukiwa ni mpango wenye lengo la
kuzoeana na kujuana tabia.
Huu ni wakati wa kila
mwanajamii hasa wa Tanzania kuona namna gani anaweza kumfurahisha mtu wake ili
kuepusha usaliti usiokuwa wa lazima.
Kama mtu anapewa kila
anachohitaji kutoka kwa mume au mke wake, yakiwamo mapenzi ya dhati, sembuse
wale wanaodhulumiwa haki ya ndoa?
Hii ni ngumu kuona
penzi la kweli ndani yao. Kama wewe ni mmoja wa watu wasiowaridhisha watu wao
katika ‘majambozi’, chunga sana.
Unaweza kuwa mlinzi
wa nyumba bila sababu za msingi. Utalala peke yako muda wote, maana hujui
makosa yako na hupendi kujifunza.
Jione mwenye makosa
kwa mtu wako na kutaka mabadiliko kuanzia sasa. Najua si kila mtu ni
mjuzi katika masuala ya mapenzi, ila sioni kwanini usifanye yale yatakayompa
raha na amani.
Ndugu msomaji wangu,
kama wewe ni miongoni mwa watu, hasa wasichana ambao wanaona wanapata woga kujihusisha
katika tendo la ndoa na watu wako, weka wazi kwa mawasiliano yetu hapo chini
ili upate mbinu za kuweza kukomboa ndoa au uhusiano wako.
Na ndio maana
tunaweka namba ya simu na barua pepe, ikiwa ni lengo la kuwekana sawa miongoni
mwetu, maana si wote wanaofurahia uhusiano wao.
Ndio hao
wanaojikunyata kitandani, wakiguswa tu wanakunja uso kama wamesikia harufu ya
kinyesi, huku wakitetemeka kwa woga.
Jichunge na tukutane
wiki ijayo.
+255 712 053949
No comments:
Post a Comment