Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
TIMU ya Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ kitaondoka
jijini Tanga Jumatatu ijayo kuelekea Moshi, mkoani Kilimanjaro, kwa ajili ya
kuweka kambi ya siku kadhaa kabla ya kukutana na JKT Oljoro kwenye mechi ya
ufunguzi ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu ujao.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union, Nassor Binslum
Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union yenye maskani
yake mkoani Tanga, Nassor Binslum, alisema kuwa timu yao imeamua kuelekea Moshi
kutokana na hali ya hewa ya mji huo kufanana na ya Arusha kama njia ya kuzoea
hali ya baridi.
Alisema uongozi wao umeshauliana na Kocha Mkuu, Hemed
Morocco ili timu yao watoke nje ya Mkoa wa Tanga ili waendelee na mazoezi yao
kwa ajili ya kuwafanya watese katika patashika ya ligi ya Tanzania Bara msimu
ujao unaoanza Agosti 24.
“Timu itaelekea Mombasa jumamosi hii kucheza mechi
moja ya kirafiki, halafu itaelekea Moshi itakapoweka kambi mpaka tarehe 24
mwezi huu watakapoingia Arisha kucheza na JKT Oljoro kwenye mechi ya ufunguzi,”
alisema Binslum.
Kutokana na usajili wa mwaka huu wapenzi wengi wa soka
Tanzania wamekuwa wakiitabiria kufanya vizuri Coastal Union kwani timu
nyingi zimeshindwa kutumia vema nafasi ya kusajili wacezaji wenye uwezo.
Coastal Union imefanikiwa kunasa wachezaji wawilai
kutoka Simba SC, wawili kutoka JKT Oljoro, mmoja ktoka Jamhuri ya Pemba, mmoja
kutoka Polisi Morogoro, mmoja kutok URA ya Uganda na mmoja kutoka Bandari ya
Mombasa wakati mwingine ametoka Azam FC.
No comments:
Post a Comment