Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
UONGOZI wa klabu ya
Yanga, umefurahia kuwasili kwa mshambuliaji wao Kimataifa, Hamis Kiiza,
akitokea nchini kwao Uganda, huku wakiingia naye mkataba wa miaka mwili kwa
ajili ya kuitumikia klabu hiyo.
Hamis Kiiza, pichani
Kiiza aliwasili juzi
jioni akitokea nyumbani kwao Uganda, huku ujio wake ukitarajiwa kuwa ndio
mwisho wa vuta nikuvute na kuwatia wasiwasi mashabiki na wadau wa timu ya
Yanga.
Akizungumza jana
jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kuwa Kiiza
amewasili na kujiunga na wenzake katika mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na
mashindano mbalimbali, ikiwa ni baada ya kuingia naye mkataba wa miaka miwili.
Alisema kuwa tayari
wameshaingia naye mkataba wa miaka miwili, huku wakiamini kuwa nyota huyo
ataendelea kuitumia timu yao kwa nguvu zote.
“Kiiza amewasili
nchini na kuingia naye mkataba wa miaka miwili, ambapo tunaamini kuwa tumekata
ngebe ya waliokuwa wakidhani hatutaweza kumsajili tena nyota huyu wa Kimataifa.
“Kwa sasa limebaki
jukumu lake na benchi la ufundi kwa ajili ya kumuandaa mchezaji huyu kwa ajili
ya kuitumikia timu yetu ya Yanga,” alisema Kizuguto.
Kiiza alishindwa
kuafikiana na Yanga mara kadhaa, ambapo hata hivyo Yanga kwa kupitia msemaji
wao walishindwa kuweka wazi kiasi cha pesa walichokubaliana dhidi ya mchezaji
huyo.
No comments:
Post a Comment