Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWIMBAJI Winfirda Josephat, maarufu kama (Recho), amesema kwamba
haoni sababu ya kupondwa na watu wasiopenda kufuata nyayo za mkali wa muziki wa
Bongo Fleva, Rehema Chalamila, Ray C.
Recho akiwajibika jukwaani
Waimbaji hao wawili wanafanana kwa sauti na aina ya uimbaji,
jambo linaloleta mvutano kwa baadhi ya mashabiki wa muziki huo hapa nchini.
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es
Salaam, Recho alisema kwamba ili msanii aweze kufika mbali lazima awe na
mkongwe anayemfuata kisanaa.
Alisema kwake yeye Ray C ndio kila kitu kwake, hivyo haoni
ubaya wa kufuata nyayo zake katika miondoko ya Bongo Fleva, ukizingatia kuwa
hawezi kuharibu ndoto zao.
"Bado naweza kubaki kama Recho na yeye ataendelea kuwa Ray C,
hivyo mashabiki wangu wana kila sababu ya kuniunga mkono ili nifikie malengo
niliyojiwekea.
"Nitaendelea kuimba kwa kiwango cha juu ili niwe bora zaidi,
bila kujali wale wanaofikiri sina sababu ya kuiga mazuri yanayofanywa na
wakongwe ndani na nje ya nchi,” alisema Recho.
Mwimbaji huyo anatokea katika taasisi ya kukuza na kulea
vipaji ya Tanzania House of Talents (THT), yenye wakali kadhaa hapa nchini,
akiwamo Barnabas, Amini, Mwasiti na wengineo.
No comments:
Post a Comment