KATIBU
wa NEC, Itikadi na Uenezi, CCM, Nape Nnauye pichani, amesema japokuwa mabadiliko ni
muhimu kwa maisha ya binadamu lakini lazima kila yanapohitajika yafanywe kwa
umakini mkubwa ili yasiwe na madhara.
hdg
Amesema
ni kutokana na sababu hiyo, ndiyo maana CCM imekuwa ikisisitiza umakini na
busara kubwa vitumike wakati huu ambao Tanzania ipo katika mchakato wa kupata
katiba mpya.
Nape
amesema miongoni mwa mambo ambayo CCM inaona kwamba lazima yatazamwe kwa
umakini na busara kubwa kabla ya hatua ya mwisho, ni kuhusu Tanzania kuwa na
serikali ngapi, ambapo rasimu ya kwanza ya Katiba inapendekeza serikali tatu.
Nape
ambaye alikuwa akizungumza wakati akifungua Kongamano la Vijana mkoani Mwanza
lililofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu (BOT) Kapripoint jijini
Mwanza, juzi, alisema, kwa upande wake CCM kuhusu kipengele hicho cha Tanzania
kuwa na serikali ngapi, msimamo wake ni serikali mbili.
"Sisi
CCM tunapotangaza msimamo wetu kwamba nchi hii inastahili kuwa ya serikali
mbili, haina maana kwamba tunadharau au kuwaona wapuuzi wanaopendekeza ziwe
tatu, la, msimamo wetu huu tunaueleza kwa hoja ili hatimaye jamii ya Watanzania
ikiziona zina mantiki watuunge mkono", alisema Nape.
Aidha
Nape alisema, umuhimu wa kuwa makini na kutumia busara katika jamii kuhitaji
mabadiliko unatokana na kwamba jamii ikiyapokea kwa pupa huambulia
yasichotarajia, ikiwemo machafuko au uongozi wasiohitaji kwa ajili ya kukidhi
matakwa yao ya maendeleo.
Nape
alisema katika pupa ya kutafuta mabadiliko, zipo baadhi ya nchi kama Misri
ambazo hadi sasa zimekosa utulivu kutokana na kupokea vibaya dhana ya
mabadiliko, wakaingia mitaani lakini bila kuchukua tahadhari, hatimaye
wamejikuta mabadiliko waliyopata nayo hawayataki tena, wanataka mengine.
Akifafanua
alisema, CCM inatambua kwamba, muundo wa serikali mbili ndio utafaa katika
kudumisha Muungano, kuliko serikali tatu ambazo CCM inaona kwamba mbali ya kuwa
mzigo zaidi kwa wananchi, pia ni kuongeza changamoto juu za zile zilizopo sasa
kwenye muungano.
No comments:
Post a Comment