JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA
YA MALIASILI NA UTALITAARIFA KWA UMMAWIZARA
YA MALIASILI NA UTALII IMEKANUSHA UVUMI KUWAWATEULE WA WAZIRI WAMESAINI POSHO
MBILI
Wizara ya Maliasili
na Utalii inakanusha uvumi ulioandikwa
Na kuchapishwa na gazeti la Raia Mwema namo tarehe 07/08/2013
ukurasa wa kwanza lililobebakichwa cha habari UFISADI kama wabunge,
wateule wa waziri wasaini poshomara mbili ikiwa na ufafanuzi kuwa yumo Ofisa
Takukuru,walipwa na taaasisiwanayoichunguza.
Taarifa
hii ilikuwa na muendelezo zaidi ukurasa wa tatu wagazeti hilo.Wizara
inasisitiza kuwa uvumi huo siyo kweli kutokana na sababu zifuatazo:
Wajumbe
wa kamati husika (iliyoundwa kuchunguza tuhuma kuhusumatumizi mabaya ya fedha
unaowahusisha watendaji wa Mamlaka yaHifadhi ya Ngorongoro) (NCAA) HAWAKULIPWA
POSHO MARAMBILI.
Malipo
waliyolipwa wajumbe wa kamati husika yalilipwa na Mamlaka yaHifadhi ya Ngorongoro
(NCAA) kama ilivyo kwenye Hadidu za Rejea zakazi husika na hawakulipwa malipo
yoyote na wizara ya maliasili na utalii.
Viwango
vya posho vilivyotumika ni kwa mujibu wa Waraka wa Serikalinamba 2 wa Mwaka
2010, Ref.Na C/AC/.17/45/01/125
Malipo
yaliyofanywa kwa wajumbe wa kamati husika yalikuwa na kibalihalali cha Waziri wa
Maliasili na Utalii Mhe. Khamis Suedi Kagasheki
Kamati
husika ilifanya kazi vizuri na kukabidhi ripoti ya awaliiliyomridhisha Waziri
Kagasheki aliyewaagiza kuifanya kazi tajwa hapo juu.Ripoti hiyo ya awali na hii ya mwisho ZITAWEKWA HADHARANI iliUmma
uelewe hali halisi ya Mamlaka ya Ngorongoro na siyo upotoshaji waRaia Mwema.
Kamati
iliyoundwa na Waziri Kagasheki ilikuwa na kazi tofauti na ilekamati ya awali
iliyowahi kuongozwa na Jaji Robert Mihayo aliyeteuliwa naaliyekuwa Waziri wa
Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige mwaka 2011.
RaiaMwema
ingejiridhisha kwa kutazama hadudi za rejea za Kamati hizo mbili.Si jambo jema
Raia Mwema kuupotosha Umma.Wizara ya Maliasili na Utalii imesikitishwa na
kitendo cha gazeti la Raia Mwema,gazeti ambalo
limejijengea sifa na kuaminiwa na jamii kwa kutoa taarifa zauhakika
zinazofuata maadili ya utoaji taarifa kwa vyombo vya habari, kuchapishahabari zinazochafua jina la Wizara, Wabunge na Serikali
kiujumla bilakujihakikishia ukweli wa taarifa hizo kutoka wizara husika.
Kwa
taarifa hii, Wizara inalitaka Gazeti la Raia Mwema kufuta uvumiwaliochapisha kwenye
gazeti lao kama ilivyotajwa hapo juu na pia kuiomba radhiWizara ya Maliasili na Utalii kwa kuchapisha
habari ambazo si sahihi na pia
kuchafua jina la
Wizara.
IMETOLEWA NA KITENGO
CHA MAWASILIANO YA SERIKALIWIZARA YA MALIASILI NA UTALII 12/08/2013
No comments:
Post a Comment