Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NI wazi wajinga
duniani hawawezi kwisha, ndio maana kwenye jamii utashangaa kuona baadhi yao
wanafanya mambo yanayoshangaza umati.
Pamoja na
kushangaza huko, lakini watu hao hawawezi kugundua kuwa wanachofanya au
kufanyiwa kinaibua maswali kwa wengine.
Wawili wapendanao pichani.
Nasema
haya, huku nikiamini kuwa mambo hayo yapo na yataendelea kuwapo katika jamii.
Ndugu msomaji wangu, kwenye jamii yetu, wapo watu waliokuwa kwenye uhusiano wa
kimapenzi na wapenzi wao, tena wakiambiana kuwa wanapendana kwa dhati.
Lakini
sio kweli. Ni uongo tu. Kwanini nasema hivyo? Siku zote wawili hawa
wanaoambiana wanapendana kwa dhati, baadhi yao hupenda sana mapenzi ya siri.
Hawapendi
hata wengine wajuwe kwa sababu wanazojua wenyewe. Najua ndio kuna utamu
wake mapenzi ya siri, ila kwa undani zaidi inaonyesha watu wanaoamua
kufanya penzi hilo la siri hawapo huru.
Kujificha
huko ni ishara kuwa huwenda wanadanganya. Huwenda mmoja wapo yupo kwenye
uhusiano kwa zaidi ya mmoja.
Kama sio
mwanaume basi atakuwa mwanamke. Kuna uzuri wake wapenzi kuishi kwa kujiachia.
Hii hutokea kama watu hao wamejiweka wazi.
Kama
wazazi wanajua uhusiano wao kwa wale wasiokuwa watoto chini ya miaka 18,
kwanini muendelee kufanya siri?
Nani
mwingine anaogopewa? Kuna hatari kuwa ndugu yangu unaiba penzi la watu.
Inapoonekana kuwa wewe ndio mwizi utasemaje?
Hii ni
kwasababu tangu mwanzo hujakuwa mkali na kupinga hilo penzi la siri. Wakati
mwingine mtu anaulizwa juu ya ukaribu wake na mtu Fulani.
Lakini
majibu yake hushangaza wengi. Anajibu ni rafiki yake. Majibu haya hutolewa bila
kuangalia kama anayezungumza naye ni ndugu au rafiki tu.
Huu ni
uwendawazimu wa aina yake. Kuna kila sababu ya kuangalia nyendo zako msomaji
wangu. Sikatai wawili wanaweza kujificha kwa faida wanazojua wenyewe, ila
wakati mwingine wapenzi wetu hutumia nafasi hiyo kutusaliti na kutoka na
wengine.
Lazima
uwaze kwanini mtu wako anahitaji usiri zaidi katika penzi lenu? Je, hakuna njia
ya mkato anayopita mtu wako? Je, hakupotezei muda?
Unaweza
kukaa na mtu na kuendelea na penzi lenu la siri, ila baadaye unagundua kuwa
yupo kwenye uhusiano na mtu mwingine na wapo kwenye mpango wa kufunga ndoa.
Sauala
hilo litakusumbua kichwa. Lakini haya yote utakuwa umepoteza mwenyewe muda.
Mara nyingi anayefanya siri katika uhusiano wako, basi ana uwezo wa kutoka na
mwingine bila hata kujuana.
Kila mtu
anaambiwa ni rafiki. Kila mtu afiche siri. Kwanini? Wewe ni mwanafunzi? Bado ni
mdogo kiasi cha kuogopa kuwa wazi katika mapenzi?
Kama bado
ni mdogo hupaswi kabisa kuwa kwenye uhusiano na kama ni mwafunzi endelea na
shule. Acha kupoteza muda wa watu kwasababu ya uhuni wao.
Ndugu
msomaji wangu, kama wewe ni mhusika katika hilo, hebu jaribu kumgomea mpenzi
wako na umwambie muda wa kujificha umepitwa na wakati.
Mueleze
ni wakati sasa wa kuwa huru. Hii ni kwa wale waliofikia umri wa kuwa na wapenzi
au wachumba, maana ina uzuri wake.
Mwanamuziki Hussein
Jumbe aliwahi kuimba wimbo wake uliojulikana kama ‘Mapenzi ya Siri’. Ni wazi
mapenzi haya yanasumbua na hayana uhuru.
Hata kumshika mkono
mpenzi wako itakuwa ngumu kwasababu mnafanya siri. Pamoja na yote hayo, mwisho
wa siku unaweza kufa kwa presha utakapogundua kuwa mtu wako yupo kwenye
uhusiano na mtu mwingine.
Sikatai usiri huo
kama ni maridhiano ya wote wawili, lakini pia ni wakati wa kupeana ukweli wa
jambo hilo, hasa kama hakuna kizuizi cha wawili hao kuwa kwenye uhusiano.
Napinga usiri wa
wapenzi ambao hutumia fursa hiyo na kuendelea na uhuni kwa kutoka kimapenzi
licha ya kuwa kwenye uhusiano na mtu wake.
Tukutane wiki ijayo.
+255 712 053949
No comments:
Post a Comment