Nape Nnauye akizungumza jambo. Pichani juu ni mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye amewaponda Chadema na utaratibu
wanaotumia kukusanya maoni ya wananchi juu ya rasimu ya kwanza ya katiba kuwa
ni uhuni na kuwapotezea watu muda.
Nape akizungumza na waandishi wa
habari mjini Dodoma alipokuwa akielezea ratiba ya vikao vya CCM vya kitaifa
alisema,"sisi tunakutana kupitia maoni ya wanaCCM waliotoa maoni yao juu
ya rasimu ya kwanza ya katiba, lakini wakati sisi tunafanya hivyo watani zetu
wameamua kuwapotezea muda wananchi kwa kufanya uhuni wa mikutano ya hadhara
huku wakijua kuwa ni kinyume na sheria inayoongoza mijadala ya rasimu hiyo ya
katiba,"alisisitiza Nape.
Lakini Nape pia alimpongeza
mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya katiba nchini Jaji Warioba kufuatia kauli
yake kuwa atapokea maoni ya taasisi sio ya helkopta.
"Jaji warioba kawatendea
haki hawa watani, sheria inataka taasisi ikae kama baraza sio ikafanye mikutano
ya hadhara.Kasema sawa sawa, hawatapokea maoni ya helkopta ila ya taasisi sasa
sio busara hawa jamaa kuendelea kupoteza muda wa watu".
"Lakini najua wataendelea tu
kwasababu inabidi watoe hesabu ya pesa walizopewa kwa kazi hii.Watafanyaje sasa
zaidi ya kuruka na chopa ili wakidhi matakwa ya waliowatuma,ndo tabu ya
vibaraka!"alisisitiza Nape.
Kuhusu vikao alisema sekretariete
ya CCM imekutana kwa siku tatu mjini Dodoma kuandaa kamati kuu inayokutana
kesho na Halmashauri kuu inayokutana tarehe 24 -25/08/2013.
No comments:
Post a Comment