KUNA watu ambao wanaendelea kuingia kwenye
wasiwasi mkubwa kwasababu ya kutofurahia uhusiano wao au ndoa yao kwa wale
waliofanikiwa.
Mambo Fulani Muhimu kwa watu muhimu.
Hawa ni wale wanaoshi bila hata kugundua
namna gani ya kuwafurahisha watu wao.
Ni wale ambao licha ya kutarajia makubwa
kutoka kwa wapenzi wao, ila wametumbukia katika wasiwasi wa aina yake.
Ndugu msomaji wangu, katika uhusiano wa
kimapenzi, kuna wale ambao wapo pamoja lakini wanapokuwa kwenye tendo la ndoa,
mmoja wapo haridhiki.
Matokeo hayo yanamfanya mmoja wapo kuishi
kwa mashaka, akiamini kuwa uhusiano wake utaingia kwenye utata, pale mwenzake
atakapobaini mapungufu yake.
Nasema haya kwa kuamini kuwa mambo haya
yapo kwenye jamii yetu. Sio kila mmoja anaishi kwa raha na mwenzake. Wale ambao
tangu waanze uhusiano wao wamekuwa na furaha, hasa kwasababu ya wote
kuridhishana katika hatua mbalimbali, wengine hilo ni ndoto kwao.
Pamoja na yote hayo, ikiwa wewe ndio
muathirika katika suala hilo, hupaswi kubaki kimya. Unatakiwa uliweke wazi
suala hilo kwa mwenzako.
Kuna watu wanaofanya makosa, pale
anapogundua kuwa kila siku uwezo wa mwenzake, hasa katika suala la tendo la
ndoa unazidi kushuka chini.
Kuna mengi yanayoweza kuchangia suala hilo,
hasa kuathirika kisaikolojia, ila mwisho wa siku bado wawili hao wanaweza kukaa
chini na kuliangalia kwa mapana.
Ni bora ukamuelezea mwenzako tofauti zake
zote ili iwe njia ya kufika mbali kwenye uhusiano wenu. Ni jambo baya kubaki
kimya hali ya kuwa unajua una tatizo katika mwili wako.
Huu ndio ukweli, maana mambo kama hayo
yasipoangaliwa kwa kina, huzalisha mihemko katika uhusiano.
Ikiwa wewe ni mmoja wa wale waliokuwa
kwenye uhusiano na mtu ambaye ana tatizo linalomkabiri, likiwapo hili la
kushindwa kumfikisha mwenzako kileleni, basi badala ya kubaki kimya, chukua
hatua.
Ninaposema kuchukua hatua, sina maana ya
mtu huyo kutoka nje ya ndoa yake au kuwa na mpenzi wa pembeni. Unaweza
kumuelezea mwenzako tatizo lako na kujadili njia ya kupita.
Mengi yatakuja katika kikao hicho wewe na
mwenzako. Lakini baadaye majibu halisi yatapatikana. Kama una ugonjwa ulioanza
kunyemelea, pia mtagundua.
Lakini kubaki kimya ni kulifanya tatizo
hilo lizidi kuota mizizi na baadaye huwa ni sababu ya kwanza ya kuongeza
usaliti kwa kiwango kikubwa mno.
Uhusiano
una changamoto nyingi mno. Moja wapo ni pale mmoja wpao anaposhindwa kumkabiri
mwenzake na kumfikisha pale anapohitaji.
Ni
pale mmoja wapo anapogundua yupo kwenye uhusiano na mtu ambaye anaweza kumfanya
akasahau shida zake kwa kupewa raha anazohitaji.
Najua
si wote ni wajuzi na hakuna anayejua yote, ila ni bora tukafahamu changamoto
hizo kwa ajili ya kumaliza tatizo.
Unapaswa
kujiuliza maswali haya. Kwanini mpenzi wako au mke wako haridhiki. Je, unahisi
una matatizo ya kiafya yanayosababisha nguvu zako za kiume zipunguwe kama sio
kwisha kabisa?
Je, mtu wako ameanza kuligundua hilo na
kumsababishia msongo wa mawazo? Baada ya kuwaza haya, unapaswa kukaa chini ili
ubaini tatizo.
Kwa bahati nzuri, kwa wale wanaowapenda kwa
moyo wote watu wao, hatua hiyo haitakuwa kuongeza tatizo bali kulitatua,
ukizingatia kuwa ndio njia nzuri ya kuhakikisha kuwa wawili hao wanakuwa kwenye
upendo wao.
Msipoweza kulitatua jambo hilo, ni wazi
mwelekeo wake ni mbaya, maana wengi wao wameachana kwasababu suala hilo
linaweza kuzalisha usaliti, hasa pale mmoja wapo anapoamua kutafuta furaha kwa
mtu mwingine.
+255
712053949
No comments:
Post a Comment