https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, August 17, 2013

Sherehe za Cheza Kidansi zafana, burudani za aina yake zaporomoshwa na wakali Mapacha Watatu, Victoria Sound na Diamond Sound Original



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHEREHE za kutimiza mwaka mmoja wa group la Cheza Kidansi lililoasisiwa na Bernard James, mtangazaji wa Star Tv, zilifana ja katika Ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni na kuhudhuriwa na watu wengi, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge.

 Mgeni rasmi Songoro Mnyonge ambaye ni Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, akikata keki katika sherehe za mwaka wa Cheza Kidansi.

 Mgeni rasmi Songoro Mnyonge akimlisha keki mlezi na mdhamini wa Cheza Kidansi, Yusuphed Mhandeni.

Mdau wa muziki nchini. Deo Mutta Mwanatanga, akifanya vitu vyake jukwaani sambamba na Ndanda Cosovo kushoto kwake katika sherehe za kutimiza mwaka mmoja wa group la Cheza Kidansi, jana katika Ukumbi wa Vijana Social Hall, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

 Deo Mutta Mwanatanga wa kwanza kushoto akiwa sambamba na muasisi wa Cheza Kidansi, Bernard James, mlezi wao Yusuphed Mhandeni, Mgeni rasmi Songoro Mnyonge, Mkurugenzi wa bendi ya Victoria Sound, dada Sauda Mwilima na Meneja wa Twanga Pepeta, Hassan Rehani baada ya kumaliza kukata keki.

 Deo Mutta Mwanatanga akiteta jambo na Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka katika burudani hizo za Cheza Kidansi.


Mdau wa muziki wa dansi nchini, Engi Muro Mwanamachame akiangalia hali inavyoendelea katika sherehe za Cheza Kidansi zilizofanyika jana usiku Vijana Social Hall, Kinondoni.

Vijana wa Diamond Sound Original wakishambulia jukwaa.

Karima ChiChi Mhandeni, mke wa Yusuphed Mhandeni aliyebeba mkoba akisalimiana na mdau mwingine wa muziki wa dansi katika sherehe za Cheza Kidansi jana.

Mwinjuma Muumini akiimba pamoja na Khalid Chokoraa kulia kwake katika tukio la Cheza Kidansi. Wawili hao walikuwa kwenye vita ya maneno hivi karibuni.



Mkurugenzi wa Screen Masters na mmiliki wa mtandao wa Saluti5.com, Said Mdoe, akiangalia kinachoendelea katika Ukumbi huo wa Vijana Social Hall kwa ajli ya kuwaripotia wadau wake.

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ndio Mchumi wa Kata ya Makumbusho, jijini Dar es Salaam, ndio mdhamini wa tukio hilo ambapo pia anasimama kama mlezi katika group hilo lenye nia ya kujadili changamoto za muziki wa dansi na kuzipatia ufumbuzi kwa ajili ya kukuza tasnia hiyo nchini.

Bendi tatu za muziki wa dansi, Victoria Sound, Diamond Sound Original na Vijana wa Mapacha Watatu walifanya mambo makubwa kuwapatia burudani wapenzi wao.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...