Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
BONDIA wa Ngumi za
kulipwa nchini, Japhet Kaseba, amesema kwa sasa anafanya mambo kimya kimya ili
ajiweke sawa zaidi katika tasnia ya mchezo huo.
Akizungumza jana
jijini Dar es Salaam, Kaseba alisema kwamba mchezo wa masumbwi umekuwa na
changamoto nyingi, ukiwamo uhaba wa kupatikanaa mapambano yenye mguso.
Alisema licha ya
uhaba huo, kwa upande wake anaendelea na mazoezi makali, japo analazimika kupunguza
majigambo kwa kuhofia kuwapaa woga mabondia wengine.
“Nafanya mambo yangu
kimya kimya bila hata kupiga kelele ili
nisiwape woga mabondia wanaofikiria
kupambana na mimi katika siku
za usoni,” alisema Kaseba.
Kwa mujibu wa Kaseba,
sasa anasubiria matokeo ya pambano la Thomas Mashali na Mada Maugo, hasa baada
ya Maugo aliyekuwa kwenye mipango ya kucheza naye Septemba 7 kukubali kupambana
na Mashali Agosti 30 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment