Meneja Mauzo na Masoko wa Push
Mobile, Rugambo Rodney akimkabidhi funguo mbili Diana Elis Mkoba baada ya
kushinda shindano la Tamasha la Serengeti Fiesta 2012. Diana alikabidhiwa
magari mawili aina ya Vitz yenye thamani ya shs milioni 18.Katikati ni Baba
mdogo wa mshindi, Gratian Mkoba ambaye ni Rais wa chama cha Walimu Tanzania
(CWT). Mwaka huu, Kampuni hiyo itatoa magari manne, pikipiki 12 na fedha taslim
shs 100,000 ikiwa juma ya zawadi zote ni sh million 80.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Push Mobile Media Limited
itatoa zawadi za magari aina ya Vitz manne (4) na pikipiki 12 kwa mashabiki
mbali mbali watakaoshinda bahati nasibu maalum ya tamasha la Serengeti Fiesta
linalotarajiwa kuzinduliwa Jumamosi mjini Kigoma.
Meneja Masoko na Mauzo wa Push
Mobile Media, Rugambo Rodney alisema kuwa zawadi mbali ya magari na pikipiki,
pia watatoa zawadi za fedha taslim (sh 100,000) kwa mashabiki hao ambao ili
kushinda wanatakiwa kutuma neno Fiesta kwenda namba 15678 ili kuweza kushinda
gari, pikipiki au fedha taslim na unaweza kushinda tiketi ya VIP kwa kutuma
jina la msanii kwa mfano Diamond na kuacha nafasi na baadaye kuwema maoni yako
kwenda namba hiyo hiyo.
Rodney alisema kuwa mbali ya
kushinda tiketi, mshiriki atalipiwa tiketi ya ndege kuja Dar es salaam kwa
ajili ya kushiriki katika tamasha la fiesta la mwisho. Alisema kuwa wameamua
kuweza zawadi hizo nono ili kunogesha zaidi tamasha hilo ambalo kwa
kuwanufaisha mashabiki wa muziki hapa nchini.
Aliongeza kuwa wamejipanga ili
kuwashirikisha wananchi wote katika tamasha hilo kwani watatoa pia watazindua
huduma mpya ijulikanayo kwa jina la Simu TV ambapo itamwezesha mashabiki kuona
video mbali mbali za muziki na matukio mengine, kupata nyimbo mbali mbali,
kupata taarifa mbali mbali ikiwa pamoja na za michezo kwa kupitia simu ya
mkononi.
kuhusiana na zawadi za fedha, Rodney
alisema kuwa zawadi hiyo itakuwa inatolewa kila siku kwa mashabiki
watakaoshinda bahati nasibu hiyo. Alifafanua kuwa jumla ya sh milioni 80
zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili litakalodumu kwa kipindi cha
miezi mitatu.
No comments:
Post a Comment