Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAKAZI na wananchi wa Manzese
jijini Dar es Salaam, mchana wa leo ulikuwa mchungu kwao katika fujo
zilizosababisha kurushwa kwa mabomu dhidi ya wafanyabiashara waliokuwa
wamejerea katika maeneo yasiyoruhusiwa.
Daraja maarufu la Manzese jijini Dar es Salaam
Hatua hiyo imekuja siku chache
baada ya kuondoka kwa Rais wa Marekani, Barack Obama, ambaye ziara yake
Tanzania ilisababisha kuhamishwa kwa wafanyabiashara katika maeneo mbalimbali
jijini Dar es Salaam.
Shuhuda wetu alisema kuwa pilika
pilika hizo za mabomu ya Askari Polisi waliokwenda kuhakikisha kuwa
wafanyabiashara hao hawarudi katika eneo la Manzese.
“Hali ilikuwa mbaya mno ambapo
pia kurushwa kwa mabomu kulisababisha kuzua kwa taharuki ya aina yake na
baadaye kusababisha foleni kubwa kwa gari zinazotumia barabara ya Morogoro,”
alisema.
Mara baada ya Obama kurudi kwao
Marekani, wafanyabiashara ndogondogo wamerudi tena katika vijiwe vyao kuendelea
na biashara zao, ambapo serikali ya jiji imesema itahakikisha kuwa watu hao
hawarudi tena katika maeneo yasiyoruhusiwa.
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam,
Mecky Sadick, alisema jana kuwa suala la kuwabana wafanyabiashara hao wasirudi
katika maeneo yasiyoruhusiwa ni jambo la lazima pamoja na kulitunza jiji
kutokana na uchafu.
No comments:
Post a Comment