Hivi karibuni, Tanzania Football Federation
(TFF) iliunda Tanzania Premier League
chini ya Bodi yampitoBodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo Bodi
itakayokuwa imechaguliwa kidemokrasia. Bodi hii imeamua peke yake kuingia
katika mkataba wa miaka 3 (mitatu) na kampuni inayoitwa Azam Television (ambayo
ina mapromota wale wale wanaomiliki Azam
Football Club). Makubaliano ambayo Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam
Television, Kamati ya Utendaji ya YANGA inalipinga kwa nguvu zote katika
misingi ifuatayo:
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, akizungumza na waandishi wa Habari katika moja ya matukio ya kimichezo hapa Tanzania.
1. bodi ya TPL
1. bodi ya TPL
1.1 Bodi iliyoko sasa hivi
ni ya mpito ambayo ilitakiwa kutenguliwa na Bodi iliyochaguliwa kidemokrasia
kwa kupitia uchaguzi wa tarehe ……….. mwaka
huu na haitakiwi kuingia katika mikataba a miaka mingi wakati inakaribia
kuondoka katika ofisi.
1.2Bodi ya TPL iliyoko sasa
hivi haikuchaguliwa kidemokrasia.
1.3Bodi ya TPL iliyoko sasa
hivi haina mjumbe hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA.
2. utaratibu wa dunia
nzima
2.1Haijawahi kutokea katika ligi ya mpira wa miguu
ya kisasa kulazimishwa kwa Klabu inayoshindana katika
ligi kuachia haki zake za urushwaji wa michezo zichukuliwe na chombo cha habari
cha Klabu ya upinzani.
2.2
Mfumo (undertaking) ambao TPL
inataka kuanzisha kwa njia ya kulazimisha mkataba kwa YANGA iachie urushwaji wa michezo yake ya soka yarushwe na
Azam TV unatishia sana uwepo wa msingi wa ushindani katika soka ya Tanzania.
2.3
Makubalianokati ya TPL na Azam
Television kuhusu utaratibu wa malipo yanasemakwamba Klabu ya YANGA na Klabu
zingine zitakazoshiriki katika Ligi Kuu ya Tanzania watapata mgao sawa wa mapato ya urushwaji wa
michezo hii, ambayo YANGA inapinga kwa sababu kama inavyofanyika duniani kote
kwenye ligi zilizofanikiwa (angalau) kutofautisha mgawanyo wa mapato kati ya
timu kufuatana na matokeo ya mwisho wa ligi.
2.4
Kamati ya Utendaji ya YANGA
siyo tu haikubaliani na mgawanyo sawa wa mapato ambao hautofautishi kati ya timu ya kwanza katika ligi na timu ya
mwisho katika ligi, lakini pia ukosefu wa viwango (premiums) vitakavyolipwa:
2.4.1 Vilabu vya mpira vyenye ufuasi wa
washabiki wengi;
2.4.2
Vilabu vya mpira
vinavyoendeshwa na Wanachama;
2.4.3
Vilabu vya mpira
visivyopata ruzuku kutoka Serikalini n.k.
3.
MIGOGORO YA MASLAHI
3.1Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mpito ya TPL ni Mkurugenzi mwandamizi
wa Makampuni ya Azam na kwa hivyo
mazungumzo ya siri kati ya Bodi ya TPL na Azam ni ya kutiliwa mashaka.
3.2
Makampuni
ya Azam yana yanashindana kibiashara na makapuni mengi yakiwemo ya utengenezaji
wa vinywaji baridi na imeonyesha huko awali inaweka “matakwa maalum” muhimu
zaidi kuliko mprira wa miguu, kama vile
Azam F.C. hawashiriki katika Kombe la Tusker na kwa hiyo YANGA inakuwa na
msimamo kwamba kwa Azam Television kupewa leseni ya kurusha matangazo ya mpira
wa miguu inatishia biashara za washiriki wa sasa na wa baadaye wa YANGA.
3.3
Azam
na YANGA wana uadui wa kimichezo. Kumbuka, wakati MRISHO NGASSA alipotaka
kwenda YANGA, Azam F.C. walimkopesha kwa nguvu kwa Klabu ya Simba! Kwa hiyo
YANGA itahatarika kwa matangazo yenye upendeleo kama Azam Television itarusha
hewani michezo yake n.k.
4.
KUTOKUWA NA
UWAZI
4.1Mkataba
wa utangazaji wa miaka mingi unaotaka kuingiwa kati ya TPL na ambao badohaujarushwa Television
ya Azam haukushindanishwa na vyombo vingi vya habari, na vyombo ambayo wako tayari kwenye soka havikujulishwa
kuhusu fursa hii au walizuiliwa kufikisha mapendekezo yao ya maombi ya haki za
kurusha matangazo katika Ligi Kuu (Tanzania Premier League).
4.2
Ukosefu
wa uwazi wa TPL unanonyesha kuwa MoU iliyokusudiwa kuwekewa saini na TPL
haikufikishwa YANGA kwa ajili ya mapitio ya kisheria, licha ya YANGA kufanya
ombi hilo kwaTPL.
5.
Mazingatio ya
kibiashara
5.1 Mamlaka ya kuamua mzozo wowote wa mkataba wa leseni ya
utangazaji wa Ligi Kuu (Tanzania Premier Leagu) itakuwa ni Mahakama ya kisheria
na siyo FIFA. TPL inasingizia kwamba
leseni ya matangazo ambayo inakusudia kufanya kuwa ni maagizo ya FIFA na kwa
hiyo YANGA inapaswa kuukubali "lock, stock and barrel."
5.2
TPL
inaelezea kimakosa makubaliano ya leseni ya urushaji wa mchezo ya mpira inayotarajia kuingia na
Television ya Azam kama "makubaliano ya udhamini" (“sponsorship
agreement”) ambayo siyo sahihi, kwa sababu urushaji wa michezo ya mpira wa
miguu ni biashara inayotokana na maslahi ya uhusiano na hivyo
wahusika
wote ni lazima wazingatie maslahi yao ya kifedha.
Kwa mfano, moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya YANGA ni
mapato ya kiingilio ya mlangoni yatokanayo na michezo ya mpira wa miguu ambayo
urushwaji wa michezo hii itapunguza mapato haya. Kwa wastani michezo ya
YANGA Dar es Salaam huingiza makusanyo
ya mlangoni shilingi milioni 50 kwa kila mchezo na hata kushuka kidogo kwa 25%
katika mahudhurio ya mechi za YANGA zinafikia mara mbili ya mapendekezo ya
mapato takribani Sh milioni 8.3 kwa mwezi kupokelewa na YANGA kutoka mradi wa
kibiashara kati ya TPL na Azam Television. Kwa kuzingatia haya, kwamba hata
siku za nyuma kama kulikutokea fursa ya kurusha mchuano wa mpira unapochezwa,
wadau wote (Timu za mpira wa miguu, TFF na Mtangazaji) walikuwa wanaafikiana kwanza kwa pamoja
kuhusu mapato na mgawanyo wake.
Kamati
ya Utendaji ya YANGA ina maoni kwamba makubaliano yoyote ya kibiashara
yanayoihusu ni lazima iyalinde maslahi kifendha ya Klabu yake ambapo
makubaliano ya TPL / Azam Television hayaangalii na kwa hiyo, Kamati ya
Utendaji ya YANGA haitaki mchezo wake urushwe hewani na Azam Television.
Msisitizo
wa TPL kuwa lazima Azam Television irushe hewani michezo ya YANGA
linasikitisha. Kamati ya Utendaji ya YANGA haina tatizo na Vilabu vingine vya
mpira wa miguu zikiruhusu michezo yao kurushwa na Azam Television ila
haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mchezo wake wa Vodacom Premier
League katika Azam Television.
……………………………………..
(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI
Young Africans Sports Club
29 JULAI, 2013
No comments:
Post a Comment