Na Mwandishi Wetu, Handeni
MJASIRIAMALI kijana katika
kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, Vitalis William, maarufu
kama Kihiyo, alizikwa juzi katika makaburi ya kijiji hicho na kuacha simanzi
kubwa.
Mmoja wa wanakijiji wa Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, Sadiki Mbwana, ambaye ndio chanzo cha habari hii pichani.
Hiyo ni kutokana na aina ya
kifo chake pamoja na juhudi za kujikwamua katika lindi la umasikini,
akifanikiwa kufanya biashara mbalimbali katika kijiji hicho na Handeni kwa
ujumla.
Marehemu alifariki kwa ajali ya
pikipiki iliyogongana na baiskeli na kusababisha vifo vya watu wawili huku
mmoja akilazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, Magunga.
Akizungumza baada ya mazishi
hayo, mkazi wa kijiji cha Komsala, Sadiki Mbwana, alisema kifo cha Kihiyo
kimeacha majonzi makubwa kutokana na mchango wake.
Alisema akiwa na umri mdogo
usiozidi miaka 29, Kihiyo alifanya juhudi nyingi kujikwamua, ikiwamo kujiingiza
katika ujasiriamali na kuvutia wat wote kufuata nyayo zake.
“Tumeguswa sana na msiba wa
mwanakijiji mwenzetu huyu, ambaye kwa kiasi kikubwa alikuwa akifanya biashara
na maendeleo yake yalikuwa makubwa kupita kiasi.
“Nadhani tuna kila sababu ya
kuumia na msiba huu, huku tukitumia nafasi hii kujaribu kushawishiana ili
tufuate nyayo zake kwa ajili ya vijana kujikwamua katika lindi la umasikini,”
alisema.
Kwa mujibu wa Mbwana, marehemu
aliwahi kuja jijini Dar es Salaam, lakini alirudi kijijini kwao baada ya kuona
hakuwa na kazi ya kufanya, hivyo kuanza kuwekeza kijijini hapo na hatimae
kuanza kutokea peupe, baada ya kufanikiwa kununua vitu mbalimbali pamoja na
duka kubwa, huku akiwa na ndoto za kujitanua nje ya wilaya yao.
No comments:
Post a Comment