TIMU ya Wagosi wa kaya
wameendelea kutuma salamu kwa timu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara kwa
kuwachapa 1-0 Simba SC kwenye mechi ya kirafiki kujiandaa na msimu mpya wa ligi
kuu ya Vodacom.
Timu za Simba na Coastal zikijiandaa kwa mchezo huo ambao uliisha kwa wagosi wa kaya kushinda bao 1-0.
Mfungaji wa bao hilo
ni mshambuliaji Mkenya, Crispian Odula aliyesajiliwa kutoka Bandari ya Mombasa.
Mechi hiyo
iliyohudhuriwa na mashabiki wengi uwanja wa Mkwakwani, ilikuwa gumzo kwenye
viunga vya mji wa Tanga na Dar es Salaam ambapo Simba waliingia jijini hapo
wakijitapa kulipiza kisasi cha msimu uliopita baada ya kubaniwa kupata point za
bure na kutoka suluhu.
Kipindi cha kwanza
timu zote zilicheza kwa kujihami huku kukiwa na mashambulizi ya kushtukiza
ambapo mpaka dakika 45 za mwanzo hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
Kipindi cha pili
Coastal Union waliingia kwa kasi na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara kitu
kilichompa wakati mgumu golikipa wa Simba, Mganda Abel Dhaira.
Kufikia dakika ya 54
Crispian Odula anayeheshimika sana ndani ya jiji hilo alipokea pasi safi kutoka
kwa Keneth Masumbuko, akauacha udunde ndani ya eneo la hatari, akaja mchezaji
wa Simba akampiga tobo akainua macho kumuangalia Mganda Dhaira akamekaa uelekeo
gani, alipoona amekaa katikati ya lango akapiga kwenye nyavu ndogo na kuwatia
wazimu mashabiki wa Coastal Union waliojaa ndani ya uwanjani utadhani hakuna
Ramadhani.
Kitu kilichokuwa
kikisubiriwa kwa hamu ni kuona kama mchezaji chipukizi aliyetoka Coastal Union,
Ibrahim Twaha ‘Messi’ atacheza ama la, lakini kufika dakika ya 70 aliingizwa
kuongeza mashambulizi baada ya Simba kuelemewa. lakini kocha Morocco alifanya
ujanja kwa kumuingiza kijana mwenzie waliocheza pamoja timu B, Hamad Juma
‘Basmat’.
Kazi ya ‘Messi’ ikawa
imeishia hapo kwani Hamad alipewa kazi moja tu ya kuhakikisha ‘Messi’ akifika
winga ya kushoto ilipo ngome yake hapigi krosi.
Mbwana Kibacha na
Juma Nyosso wakaambiwa wahakikishe kijana huyo mwenye mbio nyingi havuki ukuta
wa Coastal Union. Mwisho akaonekana hana msaada wowote kwa timu namna
alivyodhibitiwa.
Kikosi cha Coastal
Union: Shaaban Kado, Mbwana Kibacha, Othman Bakari, Juma Said ‘Nyosso’, Marcus
Ndehele, Jerry Santo, Uhuru Suleiman, Crispian Odula, Keneth Masumbuko, Haruna Moshi
‘Boban’, na Daniel Lyanga.
Baadaye kocha mkuu wa
coastal Union akishirikiana na Ally Kidi walifanya mabadiliko kwenye
kipindi cha pili kwa kuwatoa Uhuru
Suleiman, Daniel Lyanga, Crispian Odula na Othman Bakar . Wakaingia Abdi Banda,
Suleiman Kassim ‘Selembe’, Mohammed Sudi na Hamad Juma ‘Basmat’.
Habari kwa hisani ya Coastal Union
No comments:
Post a Comment