Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MTIHANI wa uwakala wa
wachezaji (players agent) na uwakala wa mechi (match agent) wa Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Alhamisi ya Septemba 26 mwaka huu
saa 4 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura
Msemaji wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa kutakuwa na jumla ya
maswali 20 kwenye mtihani huo, 15 yanatoka FIFA kuhusiana na kanuni za
kimataifa za mpira wa miguu na matano yatatoka TFF kuhusiana na kanuni
mbalimbali zinazotawala mchezo huo nchini.
Kwa ambao wangependa
kufanya mtihani huo utakaokuwa katika lugha ya Kiingereza ambayo ni moja kati
ya lugha nne rasmi za FIFA wanatakiwa kujisajili TFF kwa ada ya dola 50 za
Marekani ambapo watapewa utaratibu na maeneo ambapo mtihani huo unalenga.
Mtihani huo utafanyika
saa 4 kamili asubuhi, na muda wa kufanya mtihani hautazidi dakika 90.
Mpaka sasa Tanzania ina
mawakala watano wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA. Mawakala hao ni John
Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully.
No comments:
Post a Comment