Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
UONGOZI wa klabu ya
Azam umesema kuwa baada ya kupata udhoefu na kushika nafasi ya pili kwa misimu
miwili mfululizo, sasa wanahitaji ubingwa wa Bara ili wapate nafasi ya
kuliwakilisha Taifa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mwenyekiti wa Azam, Said Mohamed
Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Azam, Said Mohamed, alisema kuwa msimu
utakaoanza mwezi Agosti mwaka huu, wana kila sababu ya kulitwaa taji hilo.
Alisema kuwa kwa
misimu miwili mfululizo, timu yao imeweza kuonysha soka la uhakika na kushika
nafasi ya pili, hivyo kwa sasa kila mtu anahitaji kulitwaa taji hilo.
“Hatuoni kwanini
mwaka huu tusinyakuwe ubingwa wa Tanzania Bara, maana tayari tumekomaa na tuna
uwezo wa juu wa kucheza soka la kuvutia ndani na nje ya nchi.
“Hatuna cha kupoteza
kwa sasa, hivyo naamini malengo haya yatafanyika kwa wakati na kulifanikisha,
ukizingatia kuwa kama ni ubora Azam tupo katika kundi hilo ndio maana timu zote
zinazoshiriki ligi wanapata kazi kubwa kutoka na ushindi katika mechi
tunazokutana nazo,” alisema Mohamed.
Baada ya kushika
nafasi ya pili katika ligi iliyomalizika hivi karibuni, Azam inayomiliki Uwanja
wake wa Chamazi uliopo Mbagala, jijini Dar es Salaam imekata tiketi ya
kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
No comments:
Post a Comment