Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MICHUANO ya Gambo CUP inayoendeshwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho
Gambo, inatarajia kuchezwa kesho Julai nne mwaka huu katika Uwanja wa Chuo Cha Ualimu
wilayani humo, huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa Tanga, Chiku Gallawa.
Mkuu wa Mkoa Tanga, Chiku Gallawa, amepangwa kushuhudia fainali za Gambo Cup wilayani Korogwe kesho.
Fainali hizo zinawakutanisha wakali wa soka wilayani Korogwe, timu ya
Korogwe United na Mtonga FC ambazo zote kwa pamoja zinazotarajiwa kucheza soka
la uhakika na kuleta shangwse kwa wadau wa soka wilayani humo.
DC Korogwe na muanzilishi wa mashindano ya Gambo Cup, Mrisho Gambo kushoto, akishuhudia kutolewa kwa vifaa vya mashindano hayo kutoka kwa NBM, akikabidhi kwa Ridhiwan Kikwete, mdau wa michezo aliyezindua mashindano hayo yanayomalizika kesho.
Akizungumzia hilo, Mwenyekiti wa Chama Cha Soka wilayani
Korogwe, Peter Juma, alisema kila kitu kimekamilika kwa ajili ya fainali za
mashindano hayo ya Gambo Cup, ambayo yalianzishwa maalum kwa ajili ya kuendeleza
soka.
Alisema kuwa wilaya ya Korogwe imekuwa na mwamko mkubwa katika
mpira wa miguu, hivyo kwa kuanzishwa kwa mashindano hayo chini ya DC Gambo,
wanaamini vijana wote wenye vipaji wamepata nafasi ya kuonyesha cheche zao.
Tunaomba wadau wote wajotokeze kwa wingi katika fainali za Gambo CUP
ambapo sisi tunaamini ni miongoni mwa mashindano yenye mguso wa aina yake
katika sekta ya mpira wa miguu.
Mgeni rasmi amepangwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa, ambapo
watu wote wa Korogwe watashuhudia namna gani timu hizi zinachuana vikali
katika kumpata bingwa wa mashindanoi haya ya Gambo Cup,” alisema.
Mashindano hayo yalianza mapema mwaka huu wilayani Korogwe huku
yakishirikisha timu mbalimbali wilayani humo na kuwa na msisimko wa aina yake.
No comments:
Post a Comment