Je, mzima?
NATUMIA muda huu kuwakumbusha wasanii wetu juu ya kuacha vituko
vyao mitaani, maana wao ndio vinara wakati wanajua kuwa usanii ni kioo cha
jamii.
Msanii Aunt Ezekiel akijiachia kama unavyomuona hapo.
Kwa kufanya hivyo, jamii itanufaika kutoka kwao, jambo ambalo kwa
sasa ni gumu kulipata kutoka kwa wasanii wetu wanaoishi kwa vituko na kuandikwa
vibaya magazetini.
Nasema hivi kwasababu mimi ni shabiki wa sanaa na wasanii, hivyo
inapotokea mapungufu kama haya ya kutia hawanazo siwezi kubaki kimya nikililia
maendeleo ya kazi yao.
Ni kwasababu hiyo, naomba wasanii wetu waone yale yenye kutia moyo
na kuelimisha jamii, huku vitendo vya kufanya uhuni, uvutaji wa dawa za
kulevya, uzinzi na uchafu mwingineo wauache.
Naamini kwa kufanya hayo, sisi wadau wao tutanufaika kwa kiasi
kikubwa, ukizingatia kuwa msanii anapofanya lolote, kuna wanaopenda kuwaiga kwa
sababu za aina mbalimbali.
Kwa mfano, leo msanii hata akivaa nusu uchi, akapita mtaani kwao,
basi wale wanaowaona nao wanatamani kuwa kama hao, hivyo kuonyesha hasara kubwa
katika jamii yao.
Jambo hili haliwezi kukubalika hata kidogo, ndio maana kwa mapenzi
yangu kwao nikaona niandike barua hii nikiamini kuwa ujumbe utafika kwa
hadhira.
Nitafurahi kama walengwa ambao ni wasanii pamoja na mashabiki wao
watausoma ujumbe huu na kuamua kubadilika kwa ajili ya faida ya jamii
inayowazunguuka.
Joseph Kirubo
Chalinze, mkoani Pwani.
Na wewe unaweza kutoa unachokiona, usichopenda katika jamii yako, iwe siasa, uchumi, sanaa na mengineyo kwa kututumia barua fupi kwa emai kambimbwana@yahoo.com au meseji kwa namba +255 712 053949 kisha sisi tutaandika. Pia unaweza kutuma na picha yako kama utaona inafaa na kuwekwa kila Jumamosi.
No comments:
Post a Comment