Na
Mwandishi wetu Handeni.
Mkuu
wa Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Muhingo Rweyemamu, amewaagiza Wastaafu wa
Jeshi la Polisi nchini kudumisha nidhamu waliojengewa wakiwa ndani ya Jeshi
hilo hata watakapokuwa Uraiani ili kuwa mfano mbele ya Jamii.
Katika
Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Afisa Tawala wa Wilaya ya Handeni Pendo
Magasha, pichani aliyesimama, Muhingo alisema kwa muundo wa Kijeshi, kila Askari ni mtu mwenye
nidhamu na hivyo kama atafanikiwa kufanya kazi na kustaafu kwa hiyari ni wazi
kuwa mtumishi huyo atakuwa mfano kwa wengine kwa hivyo wakawe tena mfano kwa
watu watakaoishinao huko Uraiani.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu.
Amewataka
kwenda kuwa mabalozi wema waendako kuishi na watu wengine na kwamba ipo haja ya
Wastaafu kusaidia kutoa elimu sio kwa wenzao wanaobaki kazini tu lakini pia
hata kwa wananchi wengine hasa vijana watakaokwenda kuishi nao ili kujenga
familia zenye maadili mema.
Awali
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Handeni SP. Zuberi Chembera, akizungumza kwa niaba ya
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga ACP Constantine Masawe, alisema kuwa kutokana
na utandawazi uliopo kwa sasa kuna haja ya Polisi wanaobaki kazi kubadilika
kimatendo na kwenda sambamba na mfumo uliopo huku kila mmoja wao akizingatia
maadili na kuwahudumia wananchi kwa upendo na ukarimu kuliko ilivyo zamani.
Naye
mmoja wa wastafu hao, Meja Jumbe Mohammed Saidi, akitoa shukrani, aliwataka
wenzake wanaobaki kazini kila mmoja kwa nafasi yake, ni lazima atoa huduma bora
katika kuwahudumia wananchi wanaofika vituoni kuomba msaada kwa vile siku hizi
kila mtu anajua haki zake.
Amesema
kama mwananchi atafanyiwa kinyume na matarajio yake ni lazima atalalamika na
hataona kama aliyekwenda kinyume ni mtu mwenyewe bali atapeleka lawama kwa
Jeshi zima la Polisi na kuwaona kuwa wote hawatendi haki kwa wananchi.
Katika
hafla hiyo, Wastaafu hao walipewa zawadi mbalimbali zikiwa fedha taslimu pamoja
na mabadi 25 kwa kila mmoja huku Mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Vibaoni
wilayani humo Mw. Abdi Kipacha, akiwachangia Askari hao mabati 15huku akisema
kama bila ya Askari Polisi hakuna usalama na hivyo hata yeye kazi yake ya
Uwalimu asingeweza kuifanya vizuri kwa vile watoto wahawatakwenda shuleni kama
hakuna amani.
Wastaaru
walioagwa ni Inspekta Xavery Chaula na Meja Jumbe Mohammed Saidi waliolitumikia
Jeshi la Polisi kwa muda wa miaka 35 kwa kila mmoja na Meja Gabinus Nyoka
aliyelitumia Jeshi hilo kwa muda wa miaka 36.
No comments:
Post a Comment