Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa
Handeni
MKUU wa wilaya ya Handeni,
amesema kuwa katika uwapo wake katika wilaya hiyo, atahakikisha rasilimali
nyingi zilizokuwapo hapo zinawanufaisha wananchi wa Handeni na Tanzania kwa
ujumla.
Mkuu wa wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu
Akizungumza mwishoni mwa wiki
iliyopita wilayani humo, Muhingo alisema kuna baadhi ya neema zilizoanza
kuonekana baada ya kufanyiwa utafiti, yakiwamo madini ya kutengeneza chuma.
Alisema endapo mpango huo
utafanikiwa kama utakavyopangwa, basi lazima kiwanda cha kutengenezwa kiwapo
wilayani humo kwa ajili ya kuzalisha ajira pia kwa Watanzania wote.
DC Muhingo alisema hatakubali
kuona wawekezaji hao wanatoa rasilimali hiyo na kuipeleka katika nchi zao na
baadaye kuwaletea Watanzania na kununua kwa bei ghali.
“Sitaki kusema yote
yanayoonekana katika wilaya hii, maana ni vingi mno na utajiri mkubwa, yakiwamo
madini haya ambayo yakitumiwa vizuri Taifa litazidi kusonga mbele.
“Tumeshasema na wenzetu kuwa
kama kweli kunahitajika kuchimbwa kwa madini hayo, basi na hicho kiwanda
kijengwe katika wilaya hii ili iwe chanzo cha ajira kipya,” alisema.
Wilaya ya Handeni kwa sasa
inategemea kilimo na ufugaji, huku changamoto zilizopo ni mabadiliko ya Tabia
Nchi yanayosababisha wakulima wapate msoto katika kazi zao.
No comments:
Post a Comment