Na Kambi Mbwana, Dar es
Salaam
VIKUNDI vinne vya kilimo
kutoka wilayani Kilindi mkoani Tanga, vinatarajiwa kuweka kambi ya siku nane
katika maonyesho ya Wakulima mkoani Morogoro na kwenda kuwa mfano bora wilayani
kwao.
Mkuu wa Wilaya Kilindi, mkoani Tanga, Selemani Liwowa, pichani.
Hayo yamesemwa na Mkuu
wa Wilaya ya Kilindi, DC Selemani Liwowa, alipozungumzia faida zinazoweza
kupatikana katika maonyesho hayo ya wakulima yanayofanyika Morogoro kwa Kanda
ya Mashariki.
Akizungumza zaidi,
Liwowa alisema kuwa maonyesho ya kilimo yamekuwa na tija kwa kiasi kikubwa,
hivyo anaamini kwa vikundi vyao vilivyopata nafasi hiyo vitakuwa kwenye
mazingira mazuri.
Alisema wao wilaya
wametoa ofa ya vikundi viwili, ambapo wadau wao wakuu, Shirika la World Vision nao wametoa ofa ya vikundi
vingine viwili kwa ajili ya kujumuika na wakulima wenzao.
“Katika maonyesho haya
ya wakulima, sisi tunaamini kuwa mpango huu utakuwa na mafanikio makubwa, hivyo
kinachotakiwa kufanywa kwa sasa ni kuongeza umakini kwenye kujifunza.
“Nane Nane imepangwa kwa
makundi, hivyo wilaya Kilindi inayotokea mkoani Tanga ipo katika Kanda ya Mashariki,
ambapo shughuli mbalimbali zitaonyeshwa na kujifunza kwa wakulima wetu,”
alisema.
Wilaya ya Kilindi
inatokea katika wilaya Handeni kabla ya kugawanywa na kuwa wilaya mbili, ambapo
zote zipo mkoani Tanga, chini ya Mkuu wa Mkoa wake, Chiku Gallawa.
No comments:
Post a Comment