Na Kambi Mbwana, Dar es
Salaam
UONGOZI wa klabu ya
Yanga, umesema kuwa unaamini mazoezi wanayofanya wachezaji wao katika Uwanja wa
Luyola, utawaweka katika nafasi nzuri katika michuano ijayo ya Ligi ya Tanzania
Bara msimu ujao.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto
Ligi hiyo ambayo Yanga
ndio mabingwa watetezi imepangwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu kwa
timu 14 kuwania taji hilo.
Akizungumza mapema wiki hii, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema timu yao
inafanya mazoezi kabambe kwa ajili ya kuwaweka sawa.
Alisema kwa kupitia
uhodari wa kocha wao Ernest Brandit, wana amini mambo yatakuwa mazuri katika
kuifanya timu yao itishe msimu ujao na kutetea vema taji lao.
“Timu yenye wachezaji wa
ushindi wanafanya mazoezi yao katika Uwanja wa Luyola, huku tukiamini kuwa
ubora wao utashangaza wengi.
“Lengo ni kutetea
ubingwa wetu tuliyoutwaa msimu uliopita, hivyo kwa sasa majukumu yote yapo kwa
benchi la ufundi na wachezaji kwa ujumla,” alisema.
Juzi katika mchezo wa
Kimataifa wa kirafiki, Yanga walitoka sare dhidi ya timu ya URA ya nchini
Uganda, ambayo walipocheza na Simba, waliibuka na ushindi wa bao 2-1.
No comments:
Post a Comment