Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Madagascar kuchezesha mechi kati ya
Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) itakayochezwa Jumamosi (Julai 27
mwaka huu) Uwanja wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala.
Rais wa TFF Leodgar Tenga
Waamuzi wataongozwa na
Kanoso Abdoul Ohabee wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Andirvoavonjy Pierre
Jean Eric. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Jinoro Velomanana Ferdinand huku
Andriamiharisoa Hubert Marie Bruno akiwa mwamuzi wa mezani (fourth official).
Kamishna wa mechi hiyo
ya marudiano ya raundi ya mwisho kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika
kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) ni Ismail Kamal kutoka Ethiopia.
Mechi hiyo namba 38
itachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Taifa Stars
ilipoteza mechi ya kwanza iliyochezwa Julai 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam
kwa bao 1-0.
Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Mwanza
ikijiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza
Fainali za CHAN mwakani nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment