Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA wa mchezo wa masumbwi hapa nchini, Rajabu Mhamila
‘Super D’, amesema kuwa kitendo cha kutengeneza DVD za ngumi ni hatua yake ya
kuhakikisha kuwa vijana wanajifunza masumbwi.
Kazi za Super D zilizoingia sokoni.
Alisema anaamini kuwa wengi wanaobahatika kuona CD hizo wana
uwezo wa kupata mwangaza na mahitaji ya kujikita zaidi katika mchezo wa
masumbwi na hatimae kufikia malengo yao waliyojiwekea.
Alisema kitendo cha bondia chipukizi kuwa na muda wa kukaa
na kujifunza ngumi kwa kuangalia waliyompita kiwango ni jambo lenye kutia moyo
katika harakati za mchezo wa masumbwi duniani.
Super D alisema suala hilo anaamini litasaidia kwa kiasi
kikubwa kuwapa njia nzuri wadau wa ngumi wakiwamo mabondia chipukizi wenye
malengo ya siku moja kuwika katika sekta ya mchezo wa ngumi duniani.
“Nimekuwa nikitengeneza CD mbalimbali ambazo kwa kiasi
fulani naamini zina uwezo mkubwa wa kuwapatia mwangaza vijana wote na wale
wanaopenda kufuatilia mchezo huo hapa nchini.
“Tayari nimekamilisha toleo jipya la CD za ngumi na wadau
wote wanaweza kuzipata sehemu mbalimbali, hususan katika makutano ya Uhuru na
Msimbazi au Jengo la Azam lililopo karibu na Kituo cha Polisi Gelezani,”
alisema.
Kwa mujibu wa Super D, DVD hizo zimejumuisha mapambano ya mabondia wenye uwezo wa kurusha masumbwi, akiwamo Mike Tyson, Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones, Miguel
No comments:
Post a Comment