Kampuni ya Africa Tourism Promotion Centre kwa
kushirikiana na kampuni ya Miss Tourism Tanzania Organisation, wameandaa
tamasha la kimataifa la Safri kuu ya Kitalii Tanzania “Tanzania Great Safari
Tour 2013” kuanzia Mwezi Agost hadi Septemba 2013 nchini Tanzania, kwa lengo la
kuhamasisha vita dhidi ya Ujangili wa Wanyama Pori (Uwindaji Haramu), Misitu
(Mazingira na Uvunaji Haramu wa Mazao ya Misitu), Maliasili za Baharini (Uvuvi
Haramu) , pia kuhamasisha Utalii wa Ndani na kutangaza Vivutio vya Utalii
waTanzania kitaifa na kimataifa.
Warembo wa Miss Utalii
Tamasha hilo la Safari Kuu ya Kitalii la
Tanzania Great Safari Tour 2013, litajumuisha na kuhusisha mashindando ya mbio
za Nyika za Kimataifa za ANT POACHING INTERNATIONAL MARATHON, NATIONAL PARKS
INTERNATIONAL MARATHON, WILDLIFE TOURISM INTERNATIONAL MARATHON,sambamba na
msafara mkuu wa kitalii Tanzania wa kutembelea na kupiga picha za Televisheni,
Video, Filamu na Minato za Makala, Matangazo, Magazeti, Majarida, Tovuti,
Mitandao ya Kijamii na vipindi maalum vya Televisheni, Redio na Filamu.
Tanzania ni miongoni
mwanchi chache Duniani zilizo jaliwa kuwa na vivutio vingi na vya pekee vya
Utalii Duniani, kuanzia Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba, Hifadhi za Bahari,
Maeneo ya Kihistoria, Maajabu ya Dunia, Hifadhi za Wanyama Pori na Utajili
mkubwa wa Utamaduni wa kuvutia. Ndiyo maana sekta ya Utalii nchini ni moja ya
sekta tegemezi na kiongozi katika pato la Taifa na kuingiza fedha za kigeni.
Utalii unachangia zaidi ya 18% ya pato la Tifa, 24% ya Pato la fedha za kigeni
la Taifa na zaidi ya 12% ya ajira zote nchini kila mwaka.
Serikali ya Tanzania
imekuwa ikifanya juhudi kubwa za kukuza na kuendeleza sekta ya utalii nchini,
ikiwa ni pamoja na juhudi kubwa za kutangaza Utalii na vivutio vya utalii vya
Tanzania kitaifa na kimataifa lakini pia kulinda na kuhifadhi maliasili za
Taifa za Utalii, kupitia wizara ya maliasili na utalii na mamlaka zake tanzu za
Utalii nchini,ikiwemo Bodi ya Utalii(TTB),Mamlaka ya Hifadhi za Taifa
(TANAPA),Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA), Mamlaka ya Huduma za Misitu
(Tanzania Forest Services) ,Mamalaka ya Wanyama Pori na Mamlaka ya Hifdhi ya
Mambo Kale. Juhudi hizo sasa zimezaa matunda katika kukuza utalii nchini
tofauti na miaka ya nyuma, hata hivyo pamoja na mafanikio hayo sekta ya Utalii
nchini sasa inakabiliwa na chnagamoto nyingi ,lakini kubwa ikiwa ni Ujangili wa
uwindaji Haramu na Uvunaji Haramu wa Mazao ya Misitu na Majini, lakini pia
changamoto ya Utalii wa Ndani na Utangazaji wa Vivutio vya Utalii Kitaifa na
Kimataifa.
Changamoto hizi hasa ya
Ujangili, imekuwa ni tishio kubwa kwa ustawi na ukuaji wa sekta ya Utalii
nchini, kutokana na kukua na kuongezeka kwa uwindaji haramu na uvunaji wa nyara
za maliasili za misitu na bahari, ambayo sasa imekuwa ni janga la Taifa na
tishio la kutoweka kwa baadhi ya wanyama Pori ,Viumbe Bahari na Misitu.
Tunaamini kuwa, wakati sasa umefika, tena wakati sahihi kwa sekta Binafsi
kuungana na sekta za Umma katika kupigana na kuhamasisha vita dhidi ya uwindaji
Haramu,Uvuvi Haramu na Uvunaji haramu wa Misitu nchini, lakini pia katika
kutangaza vivutio vya utalii Kitaifa na kimataifa na pia kuhamasisha utalii wa
Ndani.
Kutokana na kukua kwa sekta ya Utalii Duniani na
kuwa moja ya sekta muhimu katika uchumi Duniani, mataifa mengi duniani na
Afrika ikiwemo Tanzania na nchi jirani na Tanzania zimewekeza kwa kiasi
kikubwa na kufanikiwa sana katika ushirikiano na uungaji mkono wa hali na mali
wa juhudi za asasi binafsi za kutangaza na kupromoti utalii na vita dhidi
ya Ujangili kama Africa Tourism Promotion Centre na Miss Tourism Tanzania
Organisation.
Tanzania Great Safari Tour ni jibu na tafsiri ya
vitendo ya sera za taifa za Utalii, Wanyama Pori, Misitu na Utamaduni, ambapo
matukio ya kimataifa ya Mbio za Nyika za Ant Poaching International Marathon,
National Parks Marathon, Wildlife Tourism International Marathon, sambamba na
ziara ya washiriki wa kitaifa na kimataifa wa Tanzania Great Safari Tour,
katika Hifadhi za Taifa, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Maeneo ya
Kihistoria, Maeneo ya Kitamaduni, Maeneo ya Hifadhi za Bahari, Maeneo ya
Hifadhi za Misitu nay a Vivutio vingine vya Utalii nchini, huku wakihamasisha
vita dhidi ya UJangili, wakihamasisha Utalii wa Ndani,Utalii wa
Kitamaduni,Utalii wa Mikutano,Utalii wa Mazingira na kutangaza Vivutio vya
Utalii vya Tanzania Kitaifa na Kimataifa. Tanzania Great Safari Tour 2013, ni
Safari Kuu ya Kitalii ya Kihistoria likiambatana na ushiriki mkubwa wa vyombo
vya habari vya kitaifa na kimataifa, ambayo itawaweka na kuwakutanisha pamoja
wasanii wa kitaifa na kimataifa wa Filamu, Urembo, Mitindo, Muziki, Ngoma za
Asili na Maigizo lakini pia wanamichezo wa kitaifa na kimataifa wa Mpira wa
Miguu, Riadha, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Mikono, Mpira wa Meza, Rugby n.k
sambamba na wanadiplomasia na waandishi wa Habari wa Televisheni, Redio, Magazeti,
Makala, Majarida na Mitandao ya Kijamii kitaifa na kimataifa.
Tanzania Great Safari
Tour 2013, ni fulsa nyingine kwa Tanzania kutangaza Utalii na Kuhamasishisha
Vita Dhidi ya Uwindaji Haramu,Uvuvi Haramu, Uharibifu wa Mazingira na Ujangili
kwa Ujumla, kwani matukio yote ya Tanzania great Safari Tour 2013 yataonyeshwa
na kurushwa moja kwa moja (LIVE) kutoka Tanzania na kuonekana Duniani kote
kupitia Televisheni, Tovuti,Internet na Mitandao ya Kijamii, huku Promo DVD na
DVD za Filamu ya ziara zima zikigawanywa Katika vyombo mbalimbali vya habari na
Taasisi za Kidiplamasia,Mashirika ya ndege, Vyuo n.k Duniani kote. Matukio
katika zira hiyo ni pamoja na Mbio Live za Ant Poaching International Marathon
2013, National Parks International Marathon 2013, Wildlife Tourism
International Marathon 2013, Great Safari Wildlife Fashion & Talent Show
2013, Ant Poaching Street Carnival 2013, Great Safari Ant Poaching Sports
Bonanza 2013 na Mdahalo wa kitaifa wa Ujangili, Utalii na Utalii wa Ndani.
Washindi wa fainali za Taifa za Miss Utalii
Tanzania , watashiriki katika Tamasha hilo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya
kwenda kushiriki katika mashindano ya Dunia ya Miss Tourism World 2013 huko
Equatorial Guinea Octoba mwaka huu na Miss Tourism United Nation 2013 huko
Florida Marekani Novemba mwaka huu.
Kaulimbiu ya Tamasha la
Tanzania great Safari Tour 2013, ni “Stop Poaching, Protect Wildlife – Tourism
is Life, Culture is Living” (Piga Vita Ujangili, Linda Wanyama Pori – Utalii ni
Maisha, Utamaduni ni Uhai wa Taifa).
Asante,
Erasto Gideon Chipungahelo
Mwenyekiti Mtendaji
Africa Tourism Promotion
Centre na Miss Tourism Tanzania Organisation
No comments:
Post a Comment