https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, July 06, 2013

Mfanyakazi wa Makao Makuu ya CUF azikwa

Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akikabidhiwa daftari la michango wakati alipowasili Tabata, jijini Dar es salam, nyumbani kwa Marehemu Muharami Abdallah Shaaban Tanganyika aliyefariki juzi katika hospitali ya Amana. Marehemu alikuwa ni mfankazi ya ulinzi katika makao makuu ya CUF, Buguruni. Mwenye pama ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiandika kwenye daftari la michango. Mwenye pama ni Naibu katibu Mkuu wa CUF Mhe. Julius Mtatiro na kulia ni kaka wa marehemu Ismail.
Sehemu ya waombolezaji.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akipata chakula na waombolezaji wengine.

Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiongea machache kabla ya safari ya kuelekea makaburini kuanza. Alimsifia marehemu Tanganyika kama mmoja wa wafanyakazi waaminifu na makini waliojituma sana. Pia alisema wamepoteza askari hodari ambaye alikuwa nguzo muhimu ya ulinzi katika makao makuu ya chama hicho cha ulinzi.
 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiongoza mazishi hayo yaliyofanyika kwenye makaburi ya familia ya mama wa marehemu huko Segerea. Picha kwa hisani ya mitandao.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...