Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MCHORA katuni wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, amepata mwaliko katika ukanda wa Afrika Mashariki na kupewa nafasi ya kushiriki katika Tamasha la 10 la International Cartoon Luanda litakalo
fanyika Agosti 15 hadi 23 nchini Angola.
Mchora Katuni wa New Habari 2006 Ltd, Simon Regis kushoto, ambaye amepata mwaliko wa nchini Angola, akikabidhiwa zawadi ya mkoba kutoka kwa mwanafunzi wake wa uchoraji, Meddy Jumanne, leo jijini Dar es Salaam kama ishara ya kutambua mchango wake kisanaa.
Regis ambaye jina lake lilitolewa kupitia kurasa ya Facebook
ya Tamasha hilo na kumzungumza kuwa ndio mchora katuni pekee kutoka ukanda huu
wa Afrika Mashariki atakaye shiriki Tamasha hilo kubwa Duniani.
Regis aliambia Mtanzania alshtushwa sana na habari hizo
pindi alipozipata kupitia kwa watu wanaofatilia mtandao huo kasha alipoingia
kutazama akakuta ni kweli.
“Kiukweli kwangu ni faraja kubwa sana kwani litakuwa ndio
tamasha langu kubwa kushiriki tangu nianze kuchora Katuni, hivyo naomba
watanzania waniunge mkono katika kufanikisha hili,” alisema Regis.
Alisema kuwa kwake ameona ni kitu cha ajabu sana kwani tangu
aanze uchoraji ameweza kufanya tamasha moja tu kubwa hapa nchini lakini hilo
ndio limeweza kumpa nafasi ya kuwakilisha nchi kimataifa.
Alisema Tamasha hilo amablo litajumuisha wachoraji
mbalimbali kutoka kila pembe ya Dunia amabo wanachora katuni za magazetini.
No comments:
Post a Comment