Hali
ya amani nchini Misri imeingia katika wasiwasi mkubwa, huku ripoti zikionyesha
zaidi ya wananchi 42 wamefariki Dunia kutokana wafuasi wa Rais aliyepinduliwa
wa nchi hiyo, Mohammed Morsi kuandamana kushinikiza kiongozi wao arudishwe
madarakani.
Picha
zinaonyesha jinsi wananchi hao baadhi yao walivyofariki Dunia kutokana na
machafuko hayo nchini Misri, tangu mapinduzi hayo yalivyobarikiwa na Jeshi la nchi hiyo.
Tunataka haki ya Rais Morsi.
Maafisa
wa Afya Misri wamesema takriban watu 42 wameuawa kwa kupigwa risasi mjini Cairo
nje ya kambi ya kijeshi ambapo wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani
Mohammed Morsi walikua wamekusanyika, huku mamia mengine ya watu yakijeruhiwa
katika kadhia hizo ikiwa ni harakati za kutafuta haki kama wenyewe wanavyosikika wakipaza sauti zao juu za kumlinda kiongozi wao huyo.
Kundi
la Muslima Brotherhood limewataka raia wa Misri kuwapinga wale linawaita
wanaopokonya raia uhuru na demokrasia, huku likilaumu jeshi kwa kuwaua raia wake na kutolea mfano wa Mkuu wa Jeshi Abdel Fattah Al-Sisi kama muuaji Mkuu na kusema yeye ndio kinara mkuu na anayejaribu kuondosha uhai wa watu wa Misri wanaolilia haki, tangu rais huyo aliyechaguliwa kihalali apinduliwe.
Haya ndio matokeo ya kisiasa nchini Misri na kuzua taharuki kubwa tangu tangu mapinduzi hayo yalivyofanyika na kusababisha kutoelewana kwa pande tofauti.
No comments:
Post a Comment