Na Rajabu Athumani, Handeni
Wadau wa michezo wilayani Handeni mkoani Tanga
wameombwa kutoa ushirikiano wa kufanikisha ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu
uliopo wilayani humo ili uweze kukamilika.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wilayani
Handeni,(HDFA) Essau Ngadallah alibainisha hayo jana katika mkutano wa kuzindua
tawi la mashabiki wa timu ya Yanga wilayani humo na kusema kuwa wadau wa
michezo wilyani humo hawana budi kusaidia ujenzi huo.
Ngadallah alisema kuwa walitarajia timu ya Mgambo JKT ya
wilayani humo kuufanya uwanja huo kuwa uwanja wao wa nyumbani lakini
imeshindikana kwa msimu huu hivyo watatumia uwanja wa Mkwakwani kuwa uwanja wao
wa nyumbani.
Uwanja huo wa Azimio upo katika matengenezo kwa kuoteshwa
majani pia kutarajiwa kuwekwa majukwaa ambapo wadau wameombwa kuchangia kwani
kunahitajika kujengwa vyoo, vyumba vya kubadilishia nguo,chumba cha huduma ya
kwanza na magoli ambapo mdau yeyote yule aliyetayari anatakiwa kusaidia.
Handeni.Wadau wa michezo wilayani Handeni mkoani Tanga
wameombwa kutoa ushirikiano wa kufanikisha ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu
uliopo wilayani humo ili uweze kukamilika.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wilayani
Handeni,(HDFA) Essau Ngadallah alibainisha hayo jana katika mkutano wa kuzindua
tawi la mashabiki wa timu ya Yanga wilayani humo na kusema kuwa wadau wa
michezo wilyani humo hawana budi kusaidia ujenzi huo.
Ngadallah alisema kuwa walitarajia timu ya Mgambo jkt ya
wilayani humo kuufanya uwanja huo kuwa uwanja wao wa nyumbani lakini
imeshindikana kwa msimu huu hivyo watatumia uwanja wa Mkwakwani kuwa uwanja wao
wa nyumbani.
Uwanja huo wa Azimio upo katika matengenezo kwa kuoteshwa
majani pia kutarajiwa kuwekwa majukwaa ambapo wadau wameombwa kuchangia kwani
kunahitajika kujengwa vyoo,vyumba vya kubadilishia nguo,chumba cha huduma ya
kwanza na magoli ambapo mdau yeyote yule aliyetayari anatakiwa kusaidia.
Pia Ngadallah alisema tatizo kubwa kwasasa ni jinsi ya
kuweza kuotesha majani uwanjani hapo kwani kuna tatizo la upatikanaji wa maji
ya kutosha.
No comments:
Post a Comment