Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII chipukizi wa muziki wa kizazi kipya, maarufu kama
Bongo Fleva, Ahmad Salum, maarufu kama Mady Salu, amesema kwamba yupo kwenye
mipango ya aina yake ya kumpatia mafanikio.
Msanii Mady Salu akijiachia kama hivyo.
Mady Salu ni kati ya vijana wanne waliotamba na kundi lao la
Ngovita Clew lililokuwa na maskani yake Tandale jijini Dar es Salaam na
kufanikiwa kuachia wimbo wao wa ‘Maisha Miangaiko’.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mady Salu alisema
kwamba kwa sasa amesharekodi wimbo wake wa Tatizo ni ‘Kama Unanipenda’, wimbo
aliorekodi katika Studio za BM Records.
Alisema
kukamilika kwa wimbo huo ni safari yake ya kutafuta mafanikio katika muziki wa
kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva, huku akikumbuka msoto anaoendelea
kukumbana nao.
"Nipo sawa
katika kutafuta mafanikio ya muziki, maana ndio kipaji change na kazi
ninayoipenda sana, hivyo siwezi kuchoka kufanya bidii katika kutunga nyimbo,
tangu kusaambaratika kwa kundi letu la Ngovita Clew,” alisema.
Ngovita
Clew lilikuwa likiunganisha wasanii kadhaa, akiwamo Gungwa Man, Fico Man,
Kijino na Chiteni, ambapo wimbo wao wa kwanza wa Maisha Miangaiko haukuweza
kutamba sana licha ya kuwa na mashairi mazuri yenye kujenga jamii bora hapa
nchini.
No comments:
Post a Comment