Na Kambi Mbwana, Handeni
MKUU wa Wilaya Handeni, Muhingo
Rweyemamu, juzi alizindua sehemu ya pili ya matumizi ya ulipaji wa kodi kwa
kutumia mashine ya Electronic Fiscal Device (EFD) wilayani hapa.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, akizungumza
katika uzinduzi wa mashine za electronic za ukusanyaji wa kodi za bidhaa
mbalimbali mjini Handeni juzi. Kulia kwake ni Meneja Msaidizi wa TRA Mkoani
Tanga, Martenus Shirima na kushoto ni Meneja wa TRA Handeni, Charles Kamuhanda.
Picha na Kambi Mbwana.
Akizungumza katika uzinduzi
huo, DC Muhingo alisema kuwa mashine hozo za kulipia ushuru kieletronic ni
nzuri, huku zikiweza kuhamasisha pia matumizi ya kudai risiti.
Alisema mpango huo ambao
ulizinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete na
kuwataka wakuu wa wilaya kusimamia matumizi hayo, ni mpango pia unaoweza
kukusanya kodi kwa wafanyabiashara.
“Sisi Handeni kwa pamoja
tunazindua matumizi haya ya mashine za electronic za kulipa kodi ya bidhaa,
huku nikiamini kuwa kila mwananchi atalifanyia kazi.
“Wafanyabiashara wote wanunuwe
mashine hizi na kuzitumia kwa ufanisi, huku sisi wateja tunaponunua bidhaa
lazima tudai tiketi ili kulifanya jambo hili liwe na tija,” alisema DC Muhingo.
Naye Meneja wa TRA Wilayani
Handeni, Kamuhanda, alisema matumizi hayo ya mashine za electronic yana tija
kwa watu wote, wakiwamo wafanyabiashara.
Alisema juu ya wizi unaoweza
kutokea kwa wanaoachiwa biashara husika unaweza kukomeshwa kama mashine hizo
zitatumiwa kikamilifu na kila mmoja kudai risiti.
“Tunapofanya uhakiki wa
biashara zetu, basi mashine hizi zinaweza kutoa ukweli wote wa bidhaa
zilizouzwa kwa siku, wiki, mwezi hata mwaka mzima, hivyo ni namna gani mpango
huu ni mkombozi kwa wadau wote pamoja na Taifa kwa ujumla.
“Ni wakati wetu sasa kuingia
kwenye matumizi haya ambayo kwa kiasi kikubwa pia yataongeza ulipaji wa kodi
hasa kwa wale wafanyabiashara wasiopenda kulipa kodi,” alisema.
Katika uzinduzi huo,
wafanyabiashara wa wilaya ya Handeni walipewa elimu ya matumizi hayo ya mashine
kutoka kwa wafanyakazi wa TRA pamoja na Kampuni zinazosambaza mashine hizo.
No comments:
Post a Comment